Pata taarifa kuu

Niger : Msafara kwa kwanza wa wanajeshi wa Ufaransa kuaanza kuondoka Oktoba 10

Nairobi – Mamlaka ya mpito nchini Niger imetangaza kuwa msafara wa kwanza wa wanajeshi wa Ufaransa walioko nchini humo utaanza kuondoka Jumanne hii, ya Oktoba 10.

Tangazo hilo halielezei njia itakayotumiwa na msafara wa Ufaransa, wala unakoenda
Tangazo hilo halielezei njia itakayotumiwa na msafara wa Ufaransa, wala unakoenda © THOMAS COEX / AFP
Matangazo ya kibiashara

Akiisoma taarifa kwa vyombo vya habari jumatatu jioni kupitia televisheni inayomilikiwa na utawala wa kijeshi nchini humo, mkuu wa kamati iliyoundwa ili kufuatilia kuondoka kwa wanajeshi wa Ufaransa nchini Niger, Kanali-Meja Mamane Sani Kiaou, ni kuwa ratiba ya kuondoka kwa wanajeshi wa Ufaransa imeamuliwa" kwa makubaliano na pande zote mbili.

Hata hivyo Kwa sasa, jeshi la Ufaransa halijajibu tangazo hili.Huku mamlaka jijini Niamey ikisema kuwa shughuli za kuondoka kwa jeshi hilo itafanyika kuanzia jumanne hii ambapo  vikosi vya ulinzi na usalama vya Niger vimewekwa tayari kuwasindikiza wanajeshi hao wa Ufaransa watakapoanza kuondoka.

Kanali-Meja Mamane Sani Kiaou, ni kuwa ratiba ya kuondoka kwa wanajeshi wa Ufaransa imeamuliwa" kwa makubaliano na pande zote mbili
Kanali-Meja Mamane Sani Kiaou, ni kuwa ratiba ya kuondoka kwa wanajeshi wa Ufaransa imeamuliwa" kwa makubaliano na pande zote mbili REUTERS - Stringer .

Kwa upande mwingine, tangazo hilo halielezei njia itakayotumiwa na msafara wa Ufaransa, wala unakoenda.

Kwa sasa, jeshi la Ufaransa, ambalo RFI haikuweza kuwasiliana nalo, halijathibitisha wala kukanusha kuondoka huku nchini Niger kuanzia Jumanne hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.