Pata taarifa kuu

Niger: Algeria imesitisha juhudi za upatanishi wa mzozo wa Niamey

Nairobi – Algeria imetangaza kusitisha juhudi zake za upatanishi katika mgogoro wa kisiasa nchini Niger kufuatia mapinduzi ya kijeshi ya mwezi Julai.

Mwezi uliopita, Niger ilikubali pendekezo la Algeria na kuwa mptanishi kuhusu mzozo wa kisiasa kwenye taifa hilo kwa nia ya kurejesha uongozi wa kikatiba.
Mwezi uliopita, Niger ilikubali pendekezo la Algeria na kuwa mptanishi kuhusu mzozo wa kisiasa kwenye taifa hilo kwa nia ya kurejesha uongozi wa kikatiba. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Wizara yake ya mambo ya nje ilisema katika taarifa yake Jumatatu kwamba matamshi ya mamlaka ya Niger yameibua kile ilichosema ni maswali halali kuhusu nia yao ya kweli kuhusu suala la upatanishi wa Algeria.

Kwa sasa Algeria imesema imesitisha mpango huo kwa muda ilikutoa nafasi kwa jeshi nchini Niger kuonyesha nia ya kuendelea na upatanisho wake.

Mwezi uliopita, Niger ilikubali pendekezo la Algeria na kuwa mptanishi kuhusu mzozo wa kisiasa kwenye taifa hilo kwa nia ya kurejesha uongozi wa kikatiba.

Uongozi wa kijeshi nchini Niger umependekeza kipindi cha mpito cha miaka mitatu
Uongozi wa kijeshi nchini Niger umependekeza kipindi cha mpito cha miaka mitatu AFP - ISSOUF SANOGO

Algeria mwezi Agosti ilikuwa imependekeza kipindi cha mpito cha miezi sita chini ya uongozi wa kiraia.

Kwa upande wake, kiongozi wa kijeshi nchini Niger, Jenerali Abdourahamane Tchiani, aliyeongoza mapinduzi ya mwezi Julai, alikuwa anataka kipindi cha mpito cha miaka mitatu.

Algeria pia ilikuwa imepinga matumizi ya nguvu za kijeshi kuhusu mzozo wa Niger baada ya Jumuiya ya Ecowas kutishia kutumia nguvu za kijeshi kurejesha utawala wa kiraia kwenye taifa hilo.

Ecowas ilikuwa imetishia kutumia nguvu za kijeshi kurejesha utawala wa kiraia
Ecowas ilikuwa imetishia kutumia nguvu za kijeshi kurejesha utawala wa kiraia REUTERS - FRANCIS KOKOROKO

Rais wa Nigeria Bola Tinubu, ambaye pia ndiye mwenyekiti wa Jumuiya hiyo alikuwa amekaribisha mpango wa upatanishi wa Algeria.

Mpango huo wa Algeria kwa sasa unaonekana kukabiliwa na changamoto kutokana na matukio haya mapya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.