Pata taarifa kuu

HRW na Rwanda watofautiana kuhusu ripoti mpya ya ukandamizaji

NAIROBI – Na Jupiter Mayaka

Nembo ya shirika la kulinda haki za binadamu Human Rights Watch @HRW
Nembo ya shirika la kulinda haki za binadamu Human Rights Watch @HRW © HRW
Matangazo ya kibiashara

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch, HRW, limeituhumu nchi ya Rwanda kwa kutumia mbinu za kuwanyamazisha wakosoaji wake wanaoishi nje ya nchi.

Ripoti mpya ya shirika hilo iliyochapishwa Jumanne, Oktoba 10, kuhusu ukandamizaji huu, inadai kuwa mamlaka mjini Kigali imezua hali ya hofu miongoni mwa raia wa Rwanda na wanasiasa wa nchi hiyo wanaoishi uhamishoni. 

Mkurugenzi wa shirika hilo katika kanda ya Afrika ya Kati, Lewis Mudge, ametoa mfano wa mauaji ya aliyekuwa mkuu wa jeshi la Rwanda Jenerali, Faustin Kayumba Nyamwasa, akiwa nchini Afrika Kusini mwaka 2010.

Wapo watu waliouawa katika mazingira ya kipekee na yaliyotatanishi, lakini pia kuna kesi zinazofahamika tangu mwaka 2010 mfano mauaji ya aliyekuwa jenerali Kayumba Nyamwasa yaliyotekelezwa na watu waliotokea Kigali, kuna watu wengine wametekwa na wengine wanatishiwa kutekwa wakiwa barani Afrika na wapo watu walioko Ulaya unapata familia zao zinalengwa. 

00:40

Lewsi Mudge kuhusu Rwanda

Jenerali Nyamwasa alikuwa mafichoni nchini Afrika Kusini baada ya kutofautiani na aliyekuwa mwandani wake, Rais Paul Kagame, lakini Rwanda imekanusha kuhusika katika kifo chake.

 

Ripoti hiyo imechapishwa wakati huu mahakama ya juu ya Uingereza ikisikiliza rufaa iliyowasilishwa na serikali dhidi ya kuzuia mipango ya wakimbizi kupata hifadhi nchini Rwanda, ripoti hii ikisema kuwa Uingereza haifai kuizingatia Rwanda kama nchi salama.

Matokeo yanabainisha kuwa Rwanda si nchi ambayo Uingereza inapaswa kutegemea kushikilia viwango vya kimataifa au utawala wa sheria linapokuja suala la wanaotafuta hifadhi, amesema Yasmine Ahmed, mkurugenzi wa HRW wa Uingereza.

Kwenye ripoti hii HRW imesema iliwahoji takriban watu 150 kutoka sehemu mbalimbali na kunakili unyanyasaji dhidi ya raia wa Rwanda wanaoishi nchi za Australia, Ubelgiji, Canada, Ufaransa, Kenya, Msumbiji, Afrika Kusini, Tanzania, Uganda, Uingereza na Marekani na pia kuzungumza na jamaa zao wanaoishi nchini Rwanda.

Hata hivyo Rwanda kupitia msemaji wake Yolande Makolo imekanusha madai hayo, Makolo akilituhumu shirika la HRW kwa kuichafulia jina nchi yake.

Tathmini yoyote ya rekodi ya Rwanda katika kuendeleza haki, ustawi na utu wa Wanyarwanda katika kipindi cha miaka 29 iliyopita ingetambua maendeleo na mabadiliko ambayo yamepigwa. Rwanda haitazuiliwa na kazi hii na watendaji wenye imani mbaya wanaoendeleza ajenda ya kisiasa, amesema Makolo.

Nchi ya Rwanda ni nyumbani kwa wakimbizi zaidi ya laki moja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.