Pata taarifa kuu

Sudan Kusini: Serikali yatuhumiwa kwa kuminya uhuru wa vyombo vya habari

Nairobi – Baraza la haki za binadamu la umoja wa mataifa linaishtumu serikali ya Sudan Kusini, kuminya uhuru wa vyombo vya Habari, wanasiasa wa upinzani na wanaharakati. 

Serikali idaiwa kuwatumia maafisa wa polisi kuwanyamazisha wanahabari, wapinzani  na wanaharakati wanaojaribu kuikosoa serikali ya rais Salva Kiir
Serikali idaiwa kuwatumia maafisa wa polisi kuwanyamazisha wanahabari, wapinzani  na wanaharakati wanaojaribu kuikosoa serikali ya rais Salva Kiir AP - Gregorio Borgia
Matangazo ya kibiashara

Mwenyekiti wa Baraza hilo nchini Sudan Kusini, Yasmin Sooka, amesema serikali jijini Juba inatumia maafisa wa polisi kuwanyamazisha wanahabari, wapinzani  na wanaharakati wanaojaribu kuikosoa serikali ya rais Salva Kiir. 

“Serikali inawashambulia wanahabari, wanaharakati n ahata raia wa kawaida hasa wale wanaojadili masuala ambayo mamlaka haitaki yajadiliwe.” alisema Yasmin Sooka, Mwenyekiti wa Baraza hilo nchini Sudan Kusini.

00:25

Yasmin Sooka kuhusu Sudan

Aidha, Baraza hilo linatilia shaka maandalizi ya uchaguzi mkuu wa kwanza, kufanyika mwaka ujao, kwa kile inachosema hakuna dalili ya maandalizi, huku wapinzani wakizuiwa kufanya mikutano ya hadhara. 

Barney Afako ni kamishana wa bazara hilo.  

“Huwezi kuchagua au kuchaguliwa kwenye jamii ambayo mazingira yake ni mashaka na wasiwasi tu.” Alisema Barney Afako ni kamishana wa bazara hilo.

00:20

Barney Afako kuhusu Sudan

Hata hivyo, Sudan Kusini imeeendelea kusisitiza kuwa uchaguzi huo utafanyika kama ilivypangwa, huku chama kikuu cha upinzani cha SPLM IO kikitaka kutekelezwa kikamilifu kwa mkataba wa amani uliotiwa saini mwaka 2018 kabla ya uchaguzi huo kufanyika. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.