Pata taarifa kuu

Uchumi wa nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara kukua kwa kasi ndogo mwaka huu

Nairobi – Uchumi wa nchi zilizoko kusini mwa Jangwa la Sahara, unatarajiwa kukua kwa kasi ndogo mwaka huu, hali iliyochangiwa na kutetereka kwa uchumi wa mataifa ya Afrika Kusini, Nigeria na Angola, imeonesha ripoti ya benki ya dunia.

Aidha ripoti imeongeza kuwa, karibia raia wa Afrika milioni 12 wanaingia katika soko la ajira kila mwaka, lakini wanaoweza kuajiriwa ni watu milioni 3
Aidha ripoti imeongeza kuwa, karibia raia wa Afrika milioni 12 wanaingia katika soko la ajira kila mwaka, lakini wanaoweza kuajiriwa ni watu milioni 3 REUTERS - ELIZABETH FRANTZ
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Benki ya dunia, uchumi wa ukanda huo utakuwa kwa asilimia 2.5 mwaka 2023 kutoka asilimia 3.6 mwaka uliopita, huku ukitarajiwa kuimarika kwa asilimia 3.7 mwakani na 4.1 mwaka 2025.

Kwa upande wa pato ghafi la nchi hiyo, ripoti inasema nchi hazijarekodi ukuaji chanya tangu mwaka 2015, kutokana na bara hilo kushindwa kuendana na kasi ya ongezeko la idadi ya watu.

Aidha ripoti imeongeza kuwa, karibia raia wa Afrika milioni 12 wanaingia katika soko la ajira kila mwaka, lakini wanaoweza kuajiriwa ni watu milioni 3.

Katika hatua nyingine, mfululizo wa mapinduzi ya kijeshi kwenye baadhi ya mataifa ya Afrika Magharibi, na mizozo kwenye nchi za DRC, Ethiopia, Somalia na Sudan, yote hii imechangia kuongeza hatari kwa bara hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.