Pata taarifa kuu

Ujerumani na Israel wafikia makubaliano ya kihistoria ya kununua mfumo wa Arrow-3

Israel haijawahi kutia saini mkataba mkubwa hivyo wa kijeshi. Siku ya Alhamisi, Septemba 28, Ujerumani imetangaza kununua mfumo wa kuzuia makombora wa Arrow-3 kutoka Israel kwa euro bilioni nne. Inatosha kukamilisha ngao ya Ulaya dhidi ya kombora inayotakiwa na Berlin.

Mawaziri wa Ulinzi wa Ujerumani na Israel Boris Pistorius (kulia) na Yoav Gallant (kushoto) wakati wa mkutano na waandishi wa habari baada ya makubaliano ya uuzaji wa ngao ya kuzuia makombora ya Arrow-3, mjini Berlin, Septemba 28, 2023.
Mawaziri wa Ulinzi wa Ujerumani na Israel Boris Pistorius (kulia) na Yoav Gallant (kushoto) wakati wa mkutano na waandishi wa habari baada ya makubaliano ya uuzaji wa ngao ya kuzuia makombora ya Arrow-3, mjini Berlin, Septemba 28, 2023. AFP - TOBIAS SCHWARZ
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Berlin, Pascal Thibaut

Mkataba mkubwa zaidi wa kijeshi kuwahi kuhitimishwa na Israel umetiwa saini Alhamisi hii, Septemba 28 na Ujerumani. Berlin itapata mfumo wa kuzuia makombora wa Arrow-3 ambao unawezesha kuzuia vyomvo vya kupaa hewani kwenye mwinuko wa hadi kilomita 2,400. Uwekezaji huu, ambao utaendana na usafirishaji wa kwanza katika miaka miwili, ni sehemu ya mradi mpana wa Berlin wa ngao ya kuzuia makombora ya Ulaya.

"Makubaliano haya yanamhudu kila raia wa Israel, miaka 80 tu baada ya kumalizika kwa Vita vya Pili vya dunia na mauaji ya Holocaust," Waziri wa Ulinzi wa Israeli Yoav Gallant amesema. Waziri wa Ulinzi wa Israel ametaka kuona ishara kali katika makubaliano haya ambayo pia yanajumuisha kandarasi kubwa zaidi ya kijeshi - euro bilioni nne - katika historia ya taifa la Israel. Mwenzake wa Ujerumani, Boris Pistorius, ametaja "siku ya kihistoria kwa mataifa yetu mawili".

Mkataba huo ni jibu la Ujerumani kwa vita vya Ukraine na hitaji la Berlin kuimarisha ulinzi wake dhidi ya shambulio la kombora. Hazina maalum ya Bundeswehr ya euro bilioni 100 iliyopitishwa mwaka jana itafadhili operesheni iliyoidhinishwa na Bunge. Marekani, ambayo ilitengeneza mfumo wa ulinzi wa makombora wa Arrow-3 na Israel, ilitoa idhini kwa operesheni hiyo mwezi uliopita.

Wataalamu wana mashaka

Berlin inataka kuongeza kifaa hiki ambacho kinaweza kunasa vifaa vilivyo juu ya anga kwenye mfumo wa ulinzi wa anga wa Marekani Patriot na Iris-T inayozalishwa nchini Ujerumani. Vipengele hivi vitatu ni sehemu ya mradi wa ngao ya kuzuia makombora wa Ulaya uliowasilishwa na Berlin mwaka jana na ambayo nchi 19 zimejiunga, lakini ambayo inazusha ukosoaji kutoka kwa Ufaransa.

Wataalamu wanahoji maana ya kupata mfumo wa Israel Arrow-3 wakati Urusi kwa sasa haina makombora yanayoruka juu sana na ambapo kifaa hiki kitahitajika. Pia si wazi kuwa Arrow-3 inaweza kuingizwa katika ulinzi wa NATO.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.