Pata taarifa kuu

Afrika kusini: Mjukuu wa Nelson Mandela, Zoleka Mandela, amefariki

Mjukuu wa shujaa wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini  Afrika Kusini Nelson Mandela, Zoleka Mandela, amefariki dunia baada ya kuuguwa saratani akiwa na umri wa miaka 43, familia yake imethibitisha.

Zoleka Mandela, amefariki kutokana na ugonjwa wa saratani
Zoleka Mandela, amefariki kutokana na ugonjwa wa saratani AP - Salvatore Di Nolfi
Matangazo ya kibiashara

Anafahamika  kwa kuelezea mapambano yake ya muda mrefu dhidi ya ugonjwa huo wa saratani.

Alilazwa hospitalini Jumatatu kama sehemu ya matibabu yake na amefariki akiwa amezungukwa na marafiki na familia, kwa mujibu wa Zwelabo Mandela.

Alikuwa mtoto wa binti mdogo wa Mandela, Zindzi Mandela, na mume wake wa kwanza, Zwelibanzi Hlongwane.

Familia hiyo ilisema uchunguzi wa hivi majuzi kuhusu saratani, ulionyesha ilivyokuwa imeathiri  nyonga, ini, mapafu,  ubongo na uti wa mgongo.

"Tunaomboleza kumpoteza mjukuu mpendwa wa Mama Winnie na Madiba," Wakfu wa Nelson Mandela uliandika kwenye mitandao ya kijamii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.