Pata taarifa kuu

Morocco: Dola Bilioni 11.6 kutumika kujenga upya maeneo yalioharibiwa na tetemeko la ardhi

Mfalme wa Morocco Mohammed VI, amesema nchi yake itatumia Dolla Bilioni 11.6 kwa ajili ya kujenga upya maeneo yalioharibiwa baada ya tetemeko la ardhi la tarehe nane ya mwezi Septemba.

Sehemu kubwa ya watu waliopoteza makazi yao kwa sasa wanaishi katika kambi za muda
Sehemu kubwa ya watu waliopoteza makazi yao kwa sasa wanaishi katika kambi za muda REUTERS - NACHO DOCE
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa kiongozi huyo, pesa hizo pia zitatumika kuwasaidia zaidi ya watu milioni 4.2 katika majimbo yalioathirika pakubwa na tetemeko hilo la ardhi.

Watu waliopoteza makaazi yao wanatarajiwa kujengewa makao mapya, miundo mbinu iliyoharibika katika mkasa huo pia ikitarajiwa kufanyikwa marekebisho katika kipindi cha zaidi ya miaka mitano.

Mfalme wa Morocco Mohammed VI, amesema nchi yake itatumia Dolla Bilioni 11.6 kwa ajili ya kujenga upya maeneo yalioharibiwa baada ya tetemeko la ardhi
Mfalme wa Morocco Mohammed VI, amesema nchi yake itatumia Dolla Bilioni 11.6 kwa ajili ya kujenga upya maeneo yalioharibiwa baada ya tetemeko la ardhi © MOROCCAN AGENCY PRESS / AFP

Watu zaidi ya 2,900 waliuawa katika tetemeko la ardhi lenye uzito wa 6.8 wakati wengine zaidi ya elfu tano wakiripotiwa kujeruhiwa.

Hili ndilo limekuwa tetemeko kubwa zaidi la ardhi kuwahi tokea nchini Morocco katika kipindi cha zaidi ya miaka 60.

Maelfu ya watu nchini humo wamepoteza makazi yao baada ya tetemeko hilo la ardhi
Maelfu ya watu nchini humo wamepoteza makazi yao baada ya tetemeko hilo la ardhi © Mosa'ab Elshamy / AP

Miundo mbinu na zaidi ya nyumba elfu hamisini ziliharibiwa kwenye tukio hilo.

Hadi sasa, Morocco imepokea msaada wad olla milioni mia saba kuisaidia baada ya mkasa huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.