Pata taarifa kuu

Tetemeko la ardhi lasababisha vifo vya watu zaidi ya 1,000 nchini Morocco

Watu zaidi ya 1,000 wamepoteza maisha nchini Morocco na engine 1,204 wamejeruhiwa vibaya  baada ya kutokea kwa tetemeko la ardhi, Kusini Magharibi mwa mji wa kitalii wa Marrakesh nchini Morocco.

Tetemeko la ardhi nchini Morocco
Tetemeko la ardhi nchini Morocco Al Maghribi Al Youm via REUTERS - AL MAGHRIBI AL YOUM
Matangazo ya kibiashara

Tetemeko hilo lenye ukubwa wa richa 6.8, lilitokea usiku wa kuamkia Jumamosi katika maeneo yenye milima, kwa mujibu wa watalaam.

Miji ya pwani ya Rabat, Casablanca na Essaouira imetikiswa pia na tetemeko hilo, linaloelezwa kuwa baya zaidi kuwahi kuripotiwa nchini Morocco, huku maeneo kadhaa ya nchi jirani ya Algeria pia yakitikiswa na tetemeko hilo.

Wizara ya Mambo ya ndani inasema, watu wengine 672 wamejeruhiwa na 205 wapo kwenye hali mbaya, na inahofiwa kuwa huenda idadi ya vifo ikaongezeka.

Mtandao wa Internet umekatwa mjini Marrakesh huku umeme ukikatika baada ya tukio hilo, huku watu ambao hawajapatikana wanaoaminiwa kufunikwa kwenye vifusi vya majengo yaliyoporomoka wakitafutwa.

Rais wa Marekani Joe Biden, akiwa nchini India anakohudhuria mkutano wz G 20 amesema amesikitishwa na maafa ya watu nchini Morocco.

“Nasikitishwa sana na kilichotokea nchini Morocco, tunawaombea,” amesema.

“Marekani iko tayari kutoa msaada unaohitajika,” ameongeza.

Rais wa China, Xi Jinping naye pia ametuma salamu za rambirambi kwa wananchi wa Morocco baada ya tukio hilo.

Viongozi wa mataifa ya Ulaya pia wamekuwa wakituma salamu za pole, huku Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu, akisema  nchi yake iko tayari kuisaidia Morocco ilirejesha uhusiano wa kidiplomasia mwaka 2020.

Mwaka 2004, watu wengine 628 walipoteza maisha na wengine 926 wakajeruhiwa baada ya tetemeko lingine kutokea katika eneo la Al Hoceima Kaskazini mwa nchi hiyo. Mwaka 1960, tetemeko lenye ukubwa wa ritcha 6.7, lilisababisha vifo vya watu 12,000 katika mji wa  Agadir.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.