Pata taarifa kuu

Kikosi cha EAC kuendelea kuhudumu Mashariki ya DRC hadi Disemba

Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wamekubaliana kuongoza muda wa kuhudumu kwa kikosi cha EAC kilichotumwa kurejesha usalama mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Wanajeshi wa Kikosi cha Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACRF), kushoto, wakitazama waasi wa M23 wakiondoka katika mji wa Kibumba, DRC, Ijumaa, Disemba 23, 2022.
Wanajeshi wa Kikosi cha Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACRF), kushoto, wakitazama waasi wa M23 wakiondoka katika mji wa Kibumba, DRC, Ijumaa, Disemba 23, 2022. AP - Moses Sawasawa
Matangazo ya kibiashara

Kwenye kikao chao jijini Narobi, pembezoni mwa mkutano wa mazingira barani Afrika, viongozi hao wamesema wameamua kuongeza muda wa kikosi hicho cha pamoja hadi Disemba nane, wakisubiri ripoti ya tathmini.

Hatma ya kikosi hicho nchini DRC ilikuwa mashakani  baada ya rais Felix Tshisekedi kukikosoa, lakini mwezi Juni, jumuiya hiyo iliamua majeshi hayo yaendelee kuwepo kwa kipindi cha miezi mitatu zaidi.

Hadi sasa kikosi hicho kimeshtumiwa kutowaondoa waasi hasa wale wa M 23 katika maeneo kadhaa jimboni Kivu Kaskazini, hali ambayo imesababisha maandamano huko Goma dhidi yake na pia tume ya MONUSCO.

Maandamano ya wiki iliyopita yaligeuka ya vurugu ambapo watu zaidi ya 50 waliuawa.

Jumuiya hii ambayo ina wanachama saba, ilituma wanajeshi wake katika eneo hilo mwezi Novemba mwaka uliopita ili kukabiliana na kundi la waasi wa M23, ambalo limesababisha utovu wa usalama  katika mkoa wa Kivu Kaskazini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.