Sudan: Shambulio jipya la Anga jijini Khartoum lawauwa takribani raia 20.
Nairobi – Nchini Sudan, katika jiji kuu Khartoum, watu zaidi ya 20 wakiwemo watoto wawili wameuwawa baada ya shambulio la anga linalosemekana kutekelezwa na la jeshi .
Imechapishwa:
Kulingana na tarifa ni kuwa kuna baadhi ya miili iliyozikwa chini ya Vifusi katika eneo laKalakla al-Qubba kusini-magharibi mwa jiji hilo.
Taarifa za awali,zimeonya kuwa vifo zaidi havijarekodiwa, kwani miili haiwezi kuhamishwa hospitalini kwa sababu ilichomwa vibaya .
Jeshi la serikali na lile la wanajeshi wa Rapid Support Forces (RSF) wamekuwa wakipigania udhibiti wa mji wa Khartoum tangu Aprili 15 mwaka huu huku watu milioni 2.2 wakitoroka makazi yao ndani ya Sudan na zaidi ya nusu milioni wakitafuta hifadhi katika nchi jirani, kulingana na Umoja wa Mataifa.
Kufikia sasa watu 5,000 wameuawa, kulingana na makadirio kutoka kwa mradi wa mahali pa vita na takwimu za tukio.
Vikosi vya Wanajeshi wa Sudan vinadhibiti anga na vimefanya mashambulio ya anga ya mara kwa mara huku wapiganaji wa RSF wakitawala mitaa ya mji mkuu.
Mzozo huo ulianza baada ya mkuu wa jeshi Jenerali Abdel Fattah al-Burhan na mkuu wa RSF Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo kutofautiana kuhusu mustakabali wa nchi.