Pata taarifa kuu

Siku tano zakamilika baada ya mauaji ya zaidi ya raia 43 nchini DRC.

Nairobi – Siku ya jumatano wiki iliyopita watu zaidi ya 43 waliuawa  wakati wa maandamano dhidi ya jeshi la kulinda amani la Umoja wa Mataifa, MONUSCO yaliyopangwa na dhehebu la Mesia Wazalendo nchini DRC.

Polisi wakisambaratisha maandamano yaliyoitishwa na Kanisa Katoliki DRC, Kinshasa Januari 21, 2018.
Polisi wakisambaratisha maandamano yaliyoitishwa na Kanisa Katoliki DRC, Kinshasa Januari 21, 2018. REUTERS/Kenny Katombe
Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Mataifa, ulitoa wito kufanyika kwa uchunguzi huru, baada ya tukio hilo.Hata hivyo familia za waathiriwa zinaonekana kujawa na huzuni mwingi.

Wakiwa wanakaa chini ya hema ya maombolezo, baadhi ya vijana wa Goma wanalaani mauaji ya agosti thelathini. Bulonza Mburugu ni mkazi wa Nyabushongo akiwa amevalia nguo nyeusi kama ishara ya maombolezo. Hajamuona mwanawe kwa siku 5;

“Ana umri wa miaka 23, hadi leo sina dalili zake. Mwanangu hajapatikana tangu siku hiyo, sijui yuko hai au ni marehemu. Tulipitia hospitali na magereza, hakuna dalili zozote”

00:18

Bulonza Mburugu mkaazi DRC

Kwenye bango lao inasemekana kuwa maombolezo hayo yatamalizika siku ya mazishi hayo, siku ambayo bado haija julikana.

 

Jacques Sinzahera ni mwaharakati wa asasi za kiraia anahisi kwamba licha ya kusambazwa ujumbe umesikika na kuraia serikali kuchukua hatua madhubuti.

“Tunadai mazishi ya heshima kwa wahanga, malipo ya fidia na tunadai haki itendeke kwa sababu vikosi vya kitaifa haviwezi fanya mauaji ya kinyama hayawezi kutokea katikati ya jiji na vikosi vya watiifu na dunia nzima ibaki shwari” amesema JacqueSinzahera,mwaharakati wa asasi za kiraia.

00:16

Jacques Sinzahera ,MWANAHARAKATI DRC

Licha ya kuwepo kwa ujumbe wa serikali katika mji wa Goma, kamati ya uratibu wa kisekula na asasi za kiraia zimetangaza siku bila kazi hii leo ili kudai haki kwa Goma.

 

Kufuatia mauaji hayo, mashirika ya kiraia na yale ya kutetea haki za binadamu kama Lucha yamelaani kilichotokea na kutaka kusimamishwa kazi kwa Gavana wa kijeshi wa Kivu Kaskazini na Meya wa Goma.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.