Pata taarifa kuu

Joseph Borrell: Mapinduzi nchini Gabon ni kutokana na uchaguzi uliogubikwa na 'kasoro'

Josep Borrell, mkuu wa diplomasia wa Umoja wa Ulaya, amesisitiza leo Alhamisi juu ya tofauti kati ya mapinduzi nchini Niger, Julai 26, na Gabon, siku ya Jumatano Agosti 30. "Kwa kawaida, mapinduzi ya kijeshi sio suluhu lakini hatupaswi kusahau kwamba nchini Gabon kulikuwa na uchaguzi uliojaa dosari," aamesema, akibaini kwamba uchaguzi uliogubikwa na kasoro unaweza kutafsiriwa kama "mapinduzi ya kitaasisi".

Josep Borrell, mkuu wa diplomasia wa Umoja wa Ulaya.
Josep Borrell, mkuu wa diplomasia wa Umoja wa Ulaya. AP - Jean-Francois Badias
Matangazo ya kibiashara

Pia almefafanua kuwa hakuna mpango wa kuwahamisha raia wa Ulaya wanaoishi nchini Gabon, akisisitiza kuwa hali ni shwari. "Hatuoni hatari yoyote ya vurugu," amesema kutoka Toledo, Uhispania, kando ya mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya.

Gabon imetawaliwa kwa miaka 55 na familia ya Bongo

Wanajeshi walimwondoa mamlakani rais anayemaliza muda wake Ali Bongo Ondimba siku ya Jumatano, muda mfupi baada ya kutangazwa kuchaguliwa tena kama mkuu wa nchi, na kusababisha maandamano, huku shangwe zikirindima. Nchi hii ya Afrika ya Kati yenye utajiri wa mafuta ilitawaliwa kwa zaidi ya miaka 55 na familia ya Bongo.

Vita vya Ukraine na hali nchini Niger, ambapo wanajeshi walimpindua Rais Mohamed Bazoum mnamo Julai 26, vitakuwa kwenye ajenda ya mazungumzo katika mkutano huu huko Toledo.

Rais wa Nigeria Bola Tinubu, ambaye ni rais wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS), atashiriki katika mkutano huo, amesema mkuu wa diplomasia ya Ulaya.

Mapinduzi ya Niger yameongeza hali ya wasiwasi katika ukanda wa Sahel, ambapo serikali nyingine tatu za kiraia zimepinduliwa na jeshi tangu mwaka 2020 ambapo makundi ya wanajihadi yanadhibiti karibu maeneo yote.

'Mapinduzi ya kitaasisi'

Akihojiwa kwenye CNN muda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano wa Toledo, Josep Borrell alisisitiza kuwa hali nchini Gabon na Niger haziko "sawa" wala haeifanani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.