Pata taarifa kuu

Urusi, China na Afrika Kusini zampongeza rais Mnangagwa kwa kuchaguliwa tena

Mataifa ya Afrika Kusini, Urusi na China, yametuma pongezi kwa rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa kufuatia ushindi wake katika uchaguzi mkuu wenye utata wa wikendi iliyopita.

Baadhi ya waangalizi wa uchaguzi huo walisema kuwa zoezi hilo lilikosa kuafikia vigezo vya kimataifa na katiba ya nchi hiyo kuhusu uchaguzi
Baadhi ya waangalizi wa uchaguzi huo walisema kuwa zoezi hilo lilikosa kuafikia vigezo vya kimataifa na katiba ya nchi hiyo kuhusu uchaguzi © Philimon Bulawayo / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Hatua ya nchi hizo inakuja wakati huu Marekani ikiwa ya hivi punde kukashifu zoezi hilo la uchaguzi mkuu ambao upinzani nchini humo umetaja kama utapeli.

Marekani inasema upinzani ulidhulumiwa katika uchaguzi huo na kwamba baadhi ya matokeo yalikarabatiwa, tuhuma ambazo tume ya uchaguzi nchini humo imetupilia mbali.

Katika taarifa yake, Afrika Kusini imesema inafahamu kwamba uchaguzi huo ulifanyika katika hali ngumu ya kiuchumi ikizingatiwa kuwa Zimbabwe imeekewa vikwazo vya kiuchumi.

Baadhi ya waangalizi wa uchaguzi huo walisema kuwa zoezi hilo lilikosa kuafikia vigezo vya kimataifa na katiba ya nchi hiyo kuhusu uchaguzi.

Afrika Kusini, Urusi na China ni washirika wakuu wa Zimbabwe kuhusu masuala ya kuichumi na hatua ya mataifa hayo kuunga mkono uchaguzi huo,imetajwa kuwa hatua kubwa kwa nchi hiyo inayokabiliwa na tishio la kuekewa vikwazo zaidi haswa kutokana na uchaguzi huo mkuu ambao umekashifiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.