Pata taarifa kuu

Sudan: RSF inasema inaunga mkono mpango wa kusitisha vita

Nchini Sudan, Kikosi maalum cha RSF, kimesema kinaunga mkono mpango wa usitishwaji wa mapigano wa kudumu hatua ambayo huenda ikatoa matumaini ya kuwepo mazungumzo ya ana kwa kati ya pande zinazohasimiana.

Dagalo amesisitiza haja kupatikana mwafaka wa makubaliano ya amani ya kudumu
Dagalo amesisitiza haja kupatikana mwafaka wa makubaliano ya amani ya kudumu REUTERS - MOHAMED NURELDIN ABDALLAH
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake kiongozi wa RSF Jenerali, Mohamed Hamdan Dagalo, alionekana kulegeza kamba na kuonesha utayari wa kuzungumza na utawala wa kijeshi,kwa ajili ya maslahi ya nchi ya Sudan.

Dagalo amesisitiza haja kupatikana mwafaka wa makubaliano ya amani ya kudumu yanayoambatana na suluhu ya kisiasa itakayoshughulikia pia chanzo cha mapigano hayo.

Katika mpango huo anaopendekeza Dagalo maarufu Sudan Reborn, kiongozi huyo ametaja matakwa matatu anayoamini yatasaidi kumaliza mzozo huo ambayo ni uongozi unaoheshimu utafauti wa makabila,jeshi moja na uchaguzi wa demokrasia.

Mkuu wa Jeshi la Sudan Jenerali Burhan na kiongozi wa RSF Jenerali  Hemedti wamekuwa wakikabiliana kuhusu suala la uongozi
Mkuu wa Jeshi la Sudan Jenerali Burhan na kiongozi wa RSF Jenerali Hemedti wamekuwa wakikabiliana kuhusu suala la uongozi

Taarifa hii ya Dagalo inajiri majuma 20 tangu kuzuka mapigano,kiongozi wa kijeshi Jenerali  Abdel Fattah al-Burhan akiwa amewasili Port Sudan katika ziara yake ya Kwanza nje .

Umoja wa Afrika unatazamiwa kuratibu mazungumzo mengine mwishoni mwa wiki hii nchini Ethiopia, baada ya mazungumzo yaliyokuwa yakiongozwa na Marekani na Saudi Arabia kuonekana kutozalisha matunda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.