Pata taarifa kuu

Rais Macron amethibitisha kuwa balozi wake angali nchini Niger

Nairobi – Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema balozi wake nchini Niger bado yupo kwenye taifa hilo la ukanda wa Sahel licha ya makataa ya uongozi wa jeshi kumtaka aondoke.

Akizungumza wakati wa kikao na mabalozi wake kuhusu sera za kigeni jijini Paris, Macron amethibitisha kuwa balozi wake Sylvain Itte alikuwa akisikiliza akiwa jijini Niamey
Akizungumza wakati wa kikao na mabalozi wake kuhusu sera za kigeni jijini Paris, Macron amethibitisha kuwa balozi wake Sylvain Itte alikuwa akisikiliza akiwa jijini Niamey via REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza wakati wa kikao na mabalozi wake kuhusu sera za kigeni jijini Paris, Macron amethibitisha kuwa balozi wake Sylvain Itte alikuwa akisikiliza akiwa jijini Niamey nchini Niger licha ya kupewa makataa ya saa 48 Ijumaa iliyopita kuondoka.

Rais Macron amesema kwamba mabalozi wa taifa lake wamekabiliwa na hali ngumu katika baadhi ya mataifa katika miezi ya hivi karibuni kutokea nchini Sudan hadi Niger.

Utawala wa rais wa Niger Mohamed Bazoum uliangushwa tarehe 16 ya mwezi Julai na bado anazuiliwa na familia yake hatua ambayo imekashifiwa vikali na Ufaransa na mataifa mengine.

Aidha rais Macron, ametoa wito wa kuimarishwa kwa juhudi za kidiplomasia za nchi yake wakati huu kukiwa na utaratibu mpya wa kufanya mambo duniani.
Aidha rais Macron, ametoa wito wa kuimarishwa kwa juhudi za kidiplomasia za nchi yake wakati huu kukiwa na utaratibu mpya wa kufanya mambo duniani. via REUTERS - POOL

Wizara ya mambo ya kigeni ya Ufaransa Ijumaa iliyopita ilitangaza kwamba balozi Itte alikuwa amepewa saa  48 kuondoka nchini Niger, kwa madai kwamba alikuwa amekataa kushirikiana na utawala wa kijeshi na kwamba msimamo wa Ufaransa ulikuwa kinyume na masilahi ya Niger.

Macron amesisitiza kwamba nchi yake haitabadilisha msimamo wake wa kulaani mapinduzi hayo na kwamba inamuunga mkono rais Bazoum, kwa msingi kuwa alikuwa amechaguliwa kwa njia ya kidemokrasia.

Aidha rais Macron, ametoa wito wa kuimarishwa kwa juhudi za kidiplomasia za nchi yake wakati huu kukiwa na utaratibu mpya wa kufanya mambo duniani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.