Pata taarifa kuu

Wasiwasi warejea tena katika mji unaowaniwa wa Las Anod

Hali ya wasiwasi imeanza kushuhudiwa tena katika mji wa Las Anod, miezi sita baada ya makabiliano makali kuzuka kuhusu mmiliki wa mji huo kati ya majimbo ya Puntland na Somaliland, nchini Somalia.

Rais wa Somaliland Muse Bihi Abdi
Rais wa Somaliland Muse Bihi Abdi © Malak Harb / AP
Matangazo ya kibiashara

Hii inajiri baada ya watu wenye silaha wanaoungwa mkono na serikali ya Mogadishu, Ijumaa iliyopita, kuvamia na kuteka kambi ya jeshi karibu na mji wa Las Anod, huku rais wa Somaliland Muse Bihi Abdi akiapa kuwa jeshi la jimbo hilo litalipa kisasi.

Abdi amekiri kuwa uvamizi huo umesababisha baadhi ya wanajeshi wa eneo hilo kuuawa huku akiwaambia watu wasitishwe na kinachoendelea.

Wasiwasi huu unakuja wakati huu wakaazi wa Las Anod, wakiendelea kuwa na kumbukumbu ya vita vilivyotokea mapêma mwaka huu, kusababisha vifo vya watu 210 na kuwaacha na wengine zaidi ya 700 na majeraha.

Mwezi Februari, Tume ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia masuala ya kibinadamu, iliripoti kuwa machafuko hayo yalisababisha watu 185,000 kuyakimbia makaazi yao, huku Madaktari wasiokuwa na mipaka wakisitisha shughuli zao katika mji huo tangu mwezi Julai.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.