Pata taarifa kuu

Ufaransa inasema jeshi nchini Niger halina mamlaka ya kumfukuza balozi

Nairobi – Ufaransa imesema utawala wa kijeshi nchini Niger hauna mamlaka yoyote ya kutoa agizo la kuondoka kwa balozi wake jijini Niamey Sylvain Itte.

Paris inasema inaendelea kutathmini hali ya usalama na namna shughuli zinaendelea katika ubalozi wake jijini Niamey
Paris inasema inaendelea kutathmini hali ya usalama na namna shughuli zinaendelea katika ubalozi wake jijini Niamey © AFP
Matangazo ya kibiashara

Matamshi ya Paris yanakuja baada ya uongozi wa kijeshi nchini Niger Ijumaa ya wiki hii kumpa balozi wa Ufaransa kuondoka katika muda wa saa 48.

Mamlaka nchini Ufaransa imesema licha ya kupata ombi la kumtaka balozi wake kuondoka, agizo hilo la jeshi linaweza tu utawala wa Niger uliochaguliwa kidemokrasia.

Ufaransa imesema utawala wa kijeshi nchini Niger hauna mamlaka yoyote ya kutoa agizo la kuondoka kwa balozi wake jijini Niamey
Ufaransa imesema utawala wa kijeshi nchini Niger hauna mamlaka yoyote ya kutoa agizo la kuondoka kwa balozi wake jijini Niamey © Stringer / Reuters

Paris inasema inaendelea kutathmini hali ya usalama na namna shughuli zinaendelea katika ubalozi wake jijini Niamey.

Kauli ya jeshi ilionekana kama kujibu hatua ya balozi wa Ufaransa huko Niamey “kukataa kujibu mwaliko” kutoka kwa waziri kuhusu mkutano wa Ijumaa na "hatua zingine za serikali ya Ufaransa kinyume na masilahi ya Niger".

Mohamed Bazoum amekuwa akizuiliwa na wanajeshi nchini Niger tangu kuangushwa kwa utawala wake
Mohamed Bazoum amekuwa akizuiliwa na wanajeshi nchini Niger tangu kuangushwa kwa utawala wake AFP - PIUS UTOMI EKPEI

Uamuzi huu unafuatia mfululizo wa kauli na maandamano ya chuki dhidi ya Ufaransa tangu jeshi la Niger lilipompindua rais Mohamed Bazoum, ambaye tangu wakati huo anazuiliwa pamoja  na familia yake.

Viongozi hao wa kijeshi wanaishutumu Paris kwa kutaka kuingilia kijeshi nchini Niger ili kuirejesha Bazoum na kudai kuwa Jumuiya ya ECOWAS inapokea maagizo kutoka kwa Ufaransa.

Ecowas ilikuwa imetishia kutumia nguvu za kijeshi kurejesha utawala wa kiraia
Ecowas ilikuwa imetishia kutumia nguvu za kijeshi kurejesha utawala wa kiraia REUTERS - FRANCIS KOKOROKO

ECOWAS imeiwekea Niger vikwazo vizito vya kiuchumi kufuatia mapinduzi hayo na imetishia kutumia nguvu kurejesha utulivu wa kikatiba huko Niger.

Ufaransa ina wanajeshi 1,500 walioko Niger kusaidia katika kupambana na makundi ya kijihadi ambayo yamekuwa yakiisumbua nchi hiyo pamoja na eneo la Sahel kwa miaka mingi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.