Pata taarifa kuu

Sudan: Mapigano kati ya jeshi na RSF kudhibiti kambi ya silaha nzito yaripotiwa

Nairobi – Mapigano makali yameshuhudiwa kati ya wanajeshi wa Sudan na wanamgambo wa RSF kudhibiti kambi ya silaha nzito, Kusini mwa jiji kuu, Khartoum.

Magenerali wawili wa jeshi wamekuwa wakiendelea na mapigano licha ya wito wa kusitishwa kutoka jamii ya kimataifa
Magenerali wawili wa jeshi wamekuwa wakiendelea na mapigano licha ya wito wa kusitishwa kutoka jamii ya kimataifa AFP - ASHRAF SHAZLY
Matangazo ya kibiashara

Kuanzia Jumapili iliyopita, wanamgambo wa RSF wamekuwa wakizingira kambi hiyo, kabla ya kuzuka kwa mapigano makali siku ya Jumatano.

Wakaazi wa mtaa wa Al-Shajara, kunakopatikana kambi hiyo, wameshuhudia makabiliano hayo, huku jeshi kupitia kiongozi wake Jenerali Abdel Fattah al-Burhan akitoa taarifa mbalimbali kuonesha kuwa limewashinda wanamgambo hao.

Upande wa wanamgambo unasema kwa kiasi kikubwa, umedhibiti kambi hiyo isipokuwa maeneo machache inayoendelea kupambana ili kuyachukua kutoka kwa wanajeshi.

Tangu kuanza vita kati ya makundi hayo mawili Aprili 15 kwa lengo la kudhibiti nchi hiyo, hakuna dalili ya utulivu kurejea, wakati huu ripoti zikieleza kuwa watu zaidi ya Elfu tano wameuawa na wengine zaidi ya Milioni 4 wameyakimbia makaazi yao na kuwaacha raia wa kawaida wakihangaika kupata misaada ya kibinadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.