Pata taarifa kuu

Jamhuri ya Afrika ya Kati: Mahakama yaidhinisha kura ya maoni kuhusu marekebisho ya katiba

Mahakama ya juu nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati, hapo jana iliidhinisha rasmi matokeo ya kura ya maoni kuhusu marekebisho ya katiba, ambapo sasa yanampa madaraka makubwa rais Faustin Archange Touadera pamoja na kugombea kwa muhula watatu ambao utakuwa ni miaka 7.

Faustin Archange Touadera, Rais wa Jamhuri ya Afrika ya kati
Faustin Archange Touadera, Rais wa Jamhuri ya Afrika ya kati AFP - LUDOVIC MARIN
Matangazo ya kibiashara

Katika uamuzi wake, mahakama imesema sehemu kubwa ya raia ambao ni asililia 95 walipiga kura kuunga mkono mpango huo, asilimia 57 ya wapiga kura wakithibitishwa kushiriki zoezi hilo.

Sheria hiyo mpya inatoa nafasi ya kuundwa kwa afisi ya makamu wa rais anayeteuliwa na rais pamoja na bunge la kitaifa, wakati lile la senet likiondolewa.

Kwa mujibu wa sheria hiyo, wanasiasa wenye uraia pacha hawaruhusiwi kugombea urais na pia inapendekeza kuongezwa kwa idadi ya majaji wa mahakama kuu kutoka tisa hadi kumi na mmoja.

Vyama vikuu vya upinzani nchini humo vilikuwa vimetoa wito wa kususiwa kwa kura hiyo ya maamuzi kwa madai kuwa ilikuwa inalenga kumpa rais Faustin-Archange Touadéra nafasi ya kusalia madarakani milele.

Wanasiasa wa upinzani waliituhumu kamati iliyopewa jukumu la kuangazia mageuzi ya katiba kwa kuchukua maagizo kutoka nchini Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.