Pata taarifa kuu

SADC yakubali kutuma wanajeshi nchini DRC

Nairobi – Viongozi wa jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC wamekubaliana kupeleka wanajeshi nchini DRC, na kuongeza muda wa ujumbe wa kijeshi wa jumuiya hiyo nchini Msumbiji, katika hatua ambayo wanasema inalenga kuleta amani katika eneo hilo.

Kikosi cha SADC kitakuwa cha tatu, baada ya kile cha Jumuiya ya Afrika Mashariki na Umoja wa Mataifa, MONUSCO
Kikosi cha SADC kitakuwa cha tatu, baada ya kile cha Jumuiya ya Afrika Mashariki na Umoja wa Mataifa, MONUSCO © LUSA
Matangazo ya kibiashara

Maazimio hayo yalitolewa baada ya Mkutano wa 43 wa Kawaida wa Wakuu wa nchi jana jijini Luanda nchini Angola.

Kikosi cha SADC kitakuwa cha tatu, baada ya kile cha Jumuiya ya Afrika Mashariki na Umoja wa Mataifa, MONUSCO.

Wadadisi wa mambo wanasema mpango wa  kupelekwa kwa kikosi cha SADC kinachopendelewa na rais Felix Tshisekedi, kitashirikiana na kile cha Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kikosi cha Jumuiya ya EAC kina hadi mwezi Septemba, kuendelea na operesheni zake, na iwapo hakitaongezewa muda na Kinshasa, huenda hatua hiyo inasukuma ujio wa kikosi cha SADC ambayo haijafahamika ni lini kitakuja.

Kauli hii ya SADC inakuja wakati katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres  akitangaza kuwa kuanzia mwezi Desemba, MONUSCO itaanzisha mchakato wa kuanza kuondoa vikosi vyake Mashariki mwa nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.