Pata taarifa kuu
SIASA-UCHAGUZI

Afrika Kusini: Vyama 7 vya upinzani vyaunda muungano kwa ajili ya uchaguzi wa 2024

Madhumuni ya muungano huu wa vyama saba vya kisiasa ni kukiangusha chama tawala cha African National Congress (ANC), madarakani tangu kumalizika kwa ubaguzi wa rangi. Azma hii ya kuunda muungano hata kabla ya uchaguzi ni kutoka chama cha kikuu cha upinzani, Democratic Alliance (DA), ambacho kinachukua takriban asilimia 20 ya kura na hivyo kuhitaji washirika ili kushinda wengi katika chama cha ANC.

Kiongozi wa chama cha upinzani cha DA John Steenhuisen mnamo Desemba 13, 2022 kwenye kikao cha Bunge la Afrika Kusini, Cape Town.
Kiongozi wa chama cha upinzani cha DA John Steenhuisen mnamo Desemba 13, 2022 kwenye kikao cha Bunge la Afrika Kusini, Cape Town. AP - Nardus Engelbrecht
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Johannesburg, Claire Bargelès

Mkutano huu wa vyama vingi ulikusudiwa kuwa wa kihistoria, na mahali mkutano huo ulifanyika hapakuchaguliwa kwa bahati mbaya: ulifanyika katika hoteli ile ile ambayo iliandaa mazungumzo ya kuvunjwa kwa ubaguzi wa rangi.

Baada ya siku mbili za majadiliano, hatimaye washiriki walitia saini kwenye hati, ikiwa na kifungu muhimu kwa wale wanaokubaliana na wazo hili lililozinduliwa na chama kikuu cha upinzani cha DA.

"Vyama vilivyopo hapa vimejitolea kuheshimu dira, vipaumbele, kanuni na mpango wa pamoja wa katiba. Na kwa hivyo hawatashiriki katika majadiliano yoyote au makubaliano ya utawala na ANC, EFF, au muundo wowote unaoshindana, "amesema William Gumede, mwezeshaji wa mkutano huo.

vyama ambavyo vimekubali kushiriki katika mmuungano huo ni poamoja na chama cha Wazulu kilichoundwa na Mangosuthu Buthelezi, chama cha kizalendo cha Afrikaner Freedom Front Plus, pamoja na Action SA cha meya wa zamani wa Johannesburg Herman Mashaba. Yote yanasimamiwa na chama cha DA, na kiongozi wake, John Steenhuisen, ambaye ametangaza:

"Hebu sote tujiandikishe ili tuweze kupiga kura, kwa mamilioni, kuwezesha mkataba huu mwaka ujao kuking'oa chama cha ANC mamlakani, na kuunda mwelekeo mpya kwa Waafrika Kusini wote, katika nchi hii nzuri. "

Vyama hivi washirika hata hivyo vitalazimika kupanua ushawishi wao mbele kidogo ili kutumaini kukiondoa chama cha ANC katika ngazi ya kitaifa. Mlango pia umeachwa wazi, ikiwa mashirika mengine, kama vile Muungano wa Kizalendo, yanataka kujiunga nao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.