Pata taarifa kuu

Watoto zaidi ya 70 wamefariki kutokana na maambukizi ya surua Sudan Kusini

Nairobi – Watoto zaidi ya 70 wamepoteza maisha kwa kipindi cha wiki tatu zilizopita nchini Sudan Kusini, kutokana na ugonjwa wa Surua.

Shirika la afya duniani limekuwa likitoa wito kwa wazazi kuhakikisha watoto wanapewa chanjo ya Surua
Shirika la afya duniani limekuwa likitoa wito kwa wazazi kuhakikisha watoto wanapewa chanjo ya Surua Reuters/Lindsey Wasson
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya afya inasema tangu kuanza kwa mwaka huu, ugonjwa huo umekuwa ukiripotiwa katika majimbo mbalimbali ya nchi hiyo, kama anavyoeleza Daktari Abdallah Faheem kutoka jimboni Jonglei.

‘‘Ugonjwa wa surua umezuka katika kaunti kadhaa na majimbo. Surua ilipozuka, magonjwa mengine kama kuharisha yanaweza kutokea. Motto anaweza kupata ugonjwa wa nimonia. Surua inaambukizwa na kuenezwa haraka kutoka binadamu hadi binadamu mwingine. Surua inasababishwa na virusi ambavyo vinaweza kubaki katika mazingara kwa masaa mawili hivi kwamba chembechembe za kuambukiza huenea na kuambukiza haraka.’’ alisema daktari Abdallah Faheem kutoka jimboni Jonglei.

00:17

Daktari Abdallah Faheem kutoka jimboni Jonglei

Jimbo la Unity pia limeathiriwa na ugonjwa. Daktari Duol Biem, anasimamia shughuli za afya katika eneo hilo.

‘‘Kampeni kubwa inaendeshwa na wafanyakazi wa wizara ya afya. Tunachohitaji sasa ni washirika wa kimataifa kutusaidia wakati huu wa kampeni. Kila mtoto anahitaji chanjo. Nawasihi wazazi wajitokeze kwa wingi na watoto wao wachanjwe.’’ alieleza Daktari Duol Biem.

00:08

Daktari Duol Biem

Madding Chuol, ni kiongozi wa serikali katika mji wa Bor, anaeleza kinachofanywa na uongozi wa nchi hiyo kudhibiti ugonjwa huo.

‘‘Lengo kuu la kampeni ya surua ni kupunguza kasi ya ueneaji wa ugonjwa huu ili kulinda wananchi wanaoweza kuupata. Mbali na kampeni ya surua kutakuwa na chanjo ya polio na kovid, hasa kwa wanaorudi Sudan kusini kutoka machafuko Sudan.’’ Madding Chuol, ni kiongozi wa serikali katika mji wa Bor. 

00:14

Madding Chuol, ni kiongozi wa serikali katika mji wa Bor

Watalaam wa afya wanaonya kuwa iwapo watoto walio chini ya umri wa miaka mitano, hawatopata lishe nzuri, itakayowasaidia kujikinga na ugonjwa huo, hali itaendelea kuwa mbaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.