Pata taarifa kuu

Waziri mkuu wa Niger amekutana na rais wa mpito wa Chad

Nairobi – Waziri mkuu wa kiraia wa Niger aliyeteuliwa na jeshi, Ali Mahaman Lamine Zeine,  na wanachama wengine wawili wa baraza la kijeshi, wamefanya ziara nchini Chad kwa mazungumzo na rais wa mpito Jenerali Mahamat Idriss Déby.

Rais wa Chad Déby amekuwa akiongoza juhudi za upatanishi kati ya jeshi nchini Niger
Rais wa Chad Déby amekuwa akiongoza juhudi za upatanishi kati ya jeshi nchini Niger © AFP
Matangazo ya kibiashara

Zeine amesema nchi yake kwa sasa inaongozwa na serikali ya mpito na kusisitiza utayari wa viongozi wa kijeshi kufanya mazungumzo.

Aidha wa waziri huyo mkuu mpya, amesisitiza kuwa licha ya nchi yake kuwa iko wazi kwa mazungumzo, watashirikiana tu na mataifa yanayoheshimu uhuru wa taifa lake.

Rais wa Chad Déby amekuwa akiongoza juhudi za upatanishi kati ya jeshi nchini Niger na serikali ya rais aliyeondolewa madarakani Mohamed Bazoum.

Rais wa Chad amekutana na waziri mkuu mpya wa Niger
Rais wa Chad amekutana na waziri mkuu mpya wa Niger © Ofisi ya rais wa Chad

Chad pia imesema haitashiriki katika mpango wowote wa kutumia nguvu za kijeshi dhidi ya utawala wa sasa wa Niamey.

Mkutano huu umefanyika wakati huu wakuu wa majeshi kutoka nchi za Ecowas wakitarajiwa kukutana jijini Accra Ghana siku ya Alhamis ya wiki hii kujadili hali ya Niger.

Wakuu hao wa jeshi wanakutana kujadili kile kinachotajwa ni kupanga mikakati ya kutumia nguvu za kijeshi kumrejesha rais Bazoum madarakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.