Pata taarifa kuu

Niger: Jeshi liko tayari kutumia diplomasia kupata muafaka: Ujumbe

Nairobi – Ujumbe wa viongozi wa kidini kutoka Nigeria wanaojaribu kusuluhisha mzozo wa Niger, wanasema utawala wa Kijeshi kwenye taifa hilo, uko tayari kutafuta muafaka kwa njia ya diplomasia, wakati huu ukivutana na jumuiya ya ECOWAS.

Bazoum na familia yake wamekuwa wakizuiliwa katika makazi ya ikulu tangu alipopinduliwa Julai 26
Bazoum na familia yake wamekuwa wakizuiliwa katika makazi ya ikulu tangu alipopinduliwa Julai 26 © REUTERS/Balima Boureima/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa ujumbe wa  huo Sheikh Bala Lau ,uliokutana na uongozi wa kijeshi ,Niamey , ambapo akizungumza baada ya kikao hicho ,amesema jenerali Abdourahamane Tiani yuko tayari kwa mazungumzo ya kusaka suluhu.

Hata hivyo ,Tiani amesisitiza mapinduzi aliyoyaongoza yalikiwa na nia njema na yalilenga kukwepusha janga ambalo lingeathiri nchi jirani ikiwemo Nigeria.

Jenerali Abdourahamane Tiani- Kiongozi wa kijeshi nchini Niger
Jenerali Abdourahamane Tiani- Kiongozi wa kijeshi nchini Niger AP

ECOWAS imeiwekea vikwazo Niger, ikiwemo kusitisha ushirikiano wa kifedha, kukata umeme na kufunga mipaka yake, huku hivi karibuni wakuu wa nchi wakiagiza kuwekwa tayari kwa kikosi cha ukanda.

Kumekuwa na mgawanyiko kuhusu kutumia jeshi kumrejesha madarakani Bazoum, nchi jirani kama Mali na Burkina Faso ,zikisema mpango huo utakuwa ni sawa na kutangaza vita na mataifa hayo.

Ecowas imetishia kutumia nguvu za kijeshi iwapo utawala wa kidemokrasia hautarejeshwa
Ecowas imetishia kutumia nguvu za kijeshi iwapo utawala wa kidemokrasia hautarejeshwa © AP/Gbemiga Olamikan

Jeshi nchini Niger, hapo jana limesema litamfungulia mashtaka ya uhaini na kuhatarisha usalama wa nchi, rais wa zamani Mohamed Bazoum, huku pia wakikashifu vikwazo walivyowekewa na jumuiya ya ECOWAS.

Bazoum na familia yake wamekuwa wakizuiliwa katika makazi ya ikulu tangu alipopinduliwa Julai 26.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.