Pata taarifa kuu

Waandamanaji wapinga mpango wa Ecowas kutuma kikosi Niger

Maelfu ya wafuasi wa mapinduzi ya Niger, wameandamana kupinga hatua ya mataifa ya Afrika Magharibi ya kupeleka jeshi nchini humo, huku mkutano muhimu wa kikanda kuhusu uwezekano wa kuingilia kati kinachoendelea nchini humo ukikosa kufanyika.

Waandamanaji wameandamana nje ya kambi ya jeshi la Ufaransa nchini Niger
Waandamanaji wameandamana nje ya kambi ya jeshi la Ufaransa nchini Niger © AFP
Matangazo ya kibiashara

ECOWAS ilikuwa imeidhinisha kuwekwa tayari kwa kikosi chake kumrejesha madarakani rais aliyechaguliwa kwa njia ya kidemokrasia Mohamed Bazoum, huku mwanadiplomasia mkuu wa umoja wa ulaya akielezea wasiwasi wake kuhusu hali yake akiwa kizuizini tangu alipotimuliwa na wanachama wa walinzi wake Julai 26.

Wawakilishi wa wanachama wa nchi za Jumuiya ya Afrika Magharibi walikuwa wamepangwa kuhudhuria mkutano siku ya Jumamosi katika mji mkuu wa Ghana Accra, duru za kijeshi zilisema Ijumaa.

Lakini baadaye walisema mkutano huo umesitishwa kwa muda usiojulikana kwa "sababu za kiufundi".

Ecowas imekuwa ikitoa  wito wa kuachiwa kwa rais anayezuiliwa na jeshi
Ecowas imekuwa ikitoa wito wa kuachiwa kwa rais anayezuiliwa na jeshi AFP - STEFANO RELLANDINI

Watu wa karibu wa jumuiya hiyo ya Ecowas, wanasema mkutano huo ulikuwa unalenga kuzugumzia zaidi jinsi ya kukabiliana na kinachoendelea nchini Niger pamoja na namna ya kuandaa kikosi chake cha kijeshi.

ECOWAS bado haijatoa maelezo kuhusu kikosi hicho cha kijeshi lakini viongozi wake wamesisitiza kuwa bado wanataka suluhu la amani.

Maelfu ya wafuasi wa mapinduzi hayo waliandamana mbele ya kambi ya jeshi la Ufaransa katika mji mkuu wa Niger Niamey Ijumaa jioni. Maandamano hayo yalikuja saa chache baada ya ECOWAS kuchukua hatua kuelekea uingiliaji wa kijeshi nchini humo.

Ecowas imetishia kutumia nguvu za kijeshi iwapo utawala wa kidemokrasia hautarejeshwa
Ecowas imetishia kutumia nguvu za kijeshi iwapo utawala wa kidemokrasia hautarejeshwa © AP/Gbemiga Olamikan

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa siku ya Ijumaa alieleza wasiwasi wake kuhsu hali ya rais aliyeondolewa madarakani wa Niger, Mohamed Bazoum, na familia yake, akisema kuwa hali waliyokuwa wakizuiliwa haikuwa nzuri.

Kamishna mkuu wa umoja wa mataifa wa haki za Kibinadamu Volker Turk alisema katika taarifa yake kwamba ripoti za kuaminika ambazo wamepokea zinaonyesha kuwa kiongozi huyo huenda anakabiliwa na unyanyasaji wa kinyama na udhalilishaji, unaokiuka sheria za kimataifa za haki za binadamu.

Umoja wa mataifa unasema unaguswa na hali ambayo rais Bazoum anazuiliwa
Umoja wa mataifa unasema unaguswa na hali ambayo rais Bazoum anazuiliwa AP - Marwan Ali

Na wakuu wa jeshi la Afrika Magharibi wanapanga mkutano wiki ijayo kuandaa mipango ya uwezekano wa kuingilia kijeshi kinachoendelea nchini Niger, msemaji wa jumuiya ya kikanda ya ECOWAS alisema Ijumaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.