Pata taarifa kuu

Wakuu wa Ecowas wanakutana kujadili mzozo wa Niger

Nairobi – Wakuu wa nchi za Afrika Magharibi wanakutana kujaribu kuamua iwapo watahitajika kutumia nguvu za kijeshi au diplomasia kurejesha demokrasia nchini Niger.

Uongozi wa kijeshi nchini Niger umeonakana kupuuza wito wa Ecowas wa kurejesha utawala wa kiraia
Uongozi wa kijeshi nchini Niger umeonakana kupuuza wito wa Ecowas wa kurejesha utawala wa kiraia REUTERS - FRANCIS KOKOROKO
Matangazo ya kibiashara

Maofisa wa jeshi nchini humo bado wanamshikilia rais wa Niger aliyeondolewa madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi ambayo yameonekana kuendelea kufanyika katika ukanda huo wa Afrika Magharibi. Wakuu wa Ecowas wanakutana mjini Abuja nchini Nigeria.

Viongozi hao wamekuwa wakiendelea kutafuta suluhu ya kurejesha utawala wa kidemokrasia katika taifa hilo linaloendelea kukabiliwa na utovu wa usalama kutoka kwa makundi ya watu wenye silaha.

Mkutano unafanyika wakati huu jeshi nchini Niger likiwa limetaja baraza la mpito
Mkutano unafanyika wakati huu jeshi nchini Niger likiwa limetaja baraza la mpito © Balima Boureima / Reuters

Licha ya wito kutoka kwa jamii ya kimataifa wa kutaka kurejeshwa kwa utawala wa kiraia nchini humo, wanajeshi waliotekeleza mapinduzi hayo wameonekana kutoitikia wito huo.

Ecowas chini ya Uenyekiti wa Nigeria awali ilikuwa imetishia kutumia nguvu za kijeshi iwapo uongozi wa kiraia hautarejeshwa.

Uongozi wa ECOWAS umetaka kurejeshwa kwa utawala wa kiraia  nchini Niger
Uongozi wa ECOWAS umetaka kurejeshwa kwa utawala wa kiraia nchini Niger © AFP/Kola Sulaimon

Nchi jirani ya Mali ambayo nayo pia imekuwa ikikabiliwa na mapinduzi ya kijeshi na ambayo inaungwa mkono na mamluki wa Urusi, imeunga mkono wanajeshi walioongoza mapinduzi nchini Niger.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.