Pata taarifa kuu
MGOMO-HAKI

Tunisia: Kampuni za kuoka zaendelea na mgomo na kumtaka rais Saïed kuingilia kati

Mgogoro wa mkate unaendelea nchini Tunisia huku wamiliki wa makampuni haya wakiandamana mbele ya makao makuu ya Wizara ya Biashara.

Wamiliki wa kampuni za kuoka mikate waliogoma waandamana mbele ya majengo ya Wizara ya Biashara mjini Tunis, Agosti 7, 2023.
Wamiliki wa kampuni za kuoka mikate waliogoma waandamana mbele ya majengo ya Wizara ya Biashara mjini Tunis, Agosti 7, 2023. AFP - FETHI BELAID
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Tunis, Lilia Blaise

Siku ya Jumatatu, Agosti 7, karibu wamiliki 200 wa makampuni ya kuoka mikate ya kisasa, kwa wito wa muungano wa Conect, waliandamana mbele ya jengo la wizara ya Biashara wakitaka suala lao liweze kupatiwa suluhu. Wamekuwa kwenye mgomo tangu Agosti 1, kujibu matakwa ya Kais Saïed ambaye anataka watengeneze tu mikate ya ruzuku, ikiwa wanataka kupokea sehemu ya unga unaofadhiliwa. Mwishoni mwa wiki iliyopita, Wizara ya Biashara ilisitisha usambazaji wa unga na semolina kwa mikate hii.

"Mkate wa ruzuku, uhuru na heshima": kauli mbiu iko wazi. Jumatatu, Agosti 7, mkate wa ruzuku umesababisha migogoro mingi nchini Tunisia kati ya waokaji mikate ambao wanamiliki mikate ya kisasa ambayo hutengeneza aina hii ya mkate, lakini pia mikate maalum, tofauti na mikate ya kitamaduni au ya aina maalum ambayo imeidhinishwa tu.

Kamel Omrani ni mkuu wa muungano wa viwanda vya kuoka mikate vya kisasa huko Jendouba, kaskazini-magharibi mwa nchi. Anaweka wazi wasiwasi wake juu ya kipindi hiki cha mgogoro:

“Kusema kweli, hali si nzuri hata kidogo. Sote tumesimama, na zaidi ya yote, maoni ya umma sasa yameongezeka dhidi yetu. Hata hivyo, kando na tofauti zetu za hadhi na kampuni za kuoka mikate za kitamaduni, tunafanya kazi kama wao, tunalipa kodi zetu. Kwa hivyo kwa nini kugombanisha sekta moja dhidi ya nyingine? Kwanini serikali iamue kuendelea kusaidia viwanda vya kuoka mikate asilia, na sisi tukae kimya? »

Tangu mgomo wao wa Agosti 1, kampuni za kuoka mikate za kisasa haziwezi tena kununua unga wa ruzuku kutoka kwa serikali, kulingana na uamuzi wa Wizara ya Biashara, ambayo kwa sasa inaelekeza usambazaji wa unga kwa mikate ya kitamaduni ili kudhibiti vyema hatari za upotoshaji au uvumi. Uamuzi usio wa haki kulingana na Mohamed Jemmali, rais wa shirika la muungano wa kampuni za kuoka mikate ya kisasa, na muungano wa Conect:

"Sisi hatuko kama wale wanaodai bei iongezwe, sisi sio mashirika ya mkate. Kwangu mimi suluhu pekee ni rais atusikilize alivyowasikiliza wengine na sisi tufanye naye mazungumzo na serikali. »

Leo wako karibu 1,500 wanaokabiliwa na vitisho, na wana karibu wafanyakazi 15,000.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.