Pata taarifa kuu

Niger: Marekani inaunga mkono juhudi za ECOWAS kurejesha utulivu

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken, amesema Marekani inaunga mkono juhudi za jumuiya ya mataifa ya Afrika magharibi, ECOWAS, kurejesha utawala wa kiraia nchini Niger, Blinken akiongoze kwamba Marekani inawasiliana na washirika wake na viongozi wa ECOWAS kuhakikisha utawala wa kiraia unarejeshwa nchini Niger.

Marekani inaunga mkono juhudi za jumuiya ya mataifa ya Afrika magharibi, ECOWAS, kurejesha utawala wa kiraia nchini Niger
Marekani inaunga mkono juhudi za jumuiya ya mataifa ya Afrika magharibi, ECOWAS, kurejesha utawala wa kiraia nchini Niger © RFI
Matangazo ya kibiashara

Ecowas ilikuwa imewapa viongozi wa mapinduzi mjini Niamey makataa ya siku saba kujiuzulu la sivyo wakabiliwe na uingiliaji wa kijeshi, makataa ambayo yakamilika siku ya Jumapili.

Katika mahojiano na mwandishi wa rfi kifaransa, Mikael Ponge, Blinken hata hivyo amesema ni vyema mazungumzo kutumika kurejesha utawala wa kiraia badala ya matumizi ya nguvu

“Tunaunga mkono hatua ya ECOWAS kurejesha utulivu nchini Niger, kwa hivyo tunashirikiana kidiplomasia na ECOWAS, tunawasiliana mara kwa mara na viongozi wa Afrika pamoja na washirika wetu wa Ulaya ikiwemo Ufaransa.” alisema Antony Blinken.

00:36

Antony Blinken, Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani

Jumtatu ya wiki hii,  Ecowas ilitangaza kuwa itafanya mkutano katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja, siku ya Alhamisi kujadili hali ya kisiasa na maendeleo ya hivi karibuni nchini Niger.

Kiongozi huyo aidha alionya kwamba iwapo kundi la mamluki la Urusi Wagner litatumwa Niger, kutakuwa na ongezeko la vifo, uharibifu na kuongezeka kwa ukosefu wa usalama.

Antony Blinken amesema anaunga mkono juhudi za ECOWAS nchini Niger
Antony Blinken amesema anaunga mkono juhudi za ECOWAS nchini Niger © RFI

Afisa huyo wa serikali ya Marekani pia alipuuzilia mbali pendekezo la Urusi la kutoa nafaka ya bure kwa nchi sita za Kiafrika akielezea hatua hiyo kama ya kicheko kwa sababu ni tani 50,000 pekee ambazo zingetolewa wakati mkataba uliokwama wa nafaka ya Bahari Nyeusi ungetoa tani milioni 20 kwa nchi za kipato cha chini na cha kati.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.