Pata taarifa kuu

Niger: Jeshi limemteua waziri mkuu mpya

Kiongozi wa kijeshi nchini Niger, Jenerali Abdourahmane Tchiani, ameteua waziri wa zamani wa fedha kwenye taifa hilo kuhudumu katika nafasi ya waziri mkuu mpya kufuatia mapinduzi ya Julai 26.

Ali Mahaman Lamine ameteuliwa kuwa waziri mkuu mpya wa Niger
Ali Mahaman Lamine ameteuliwa kuwa waziri mkuu mpya wa Niger AP - J. Scott Applewhite
Matangazo ya kibiashara

Ali Mahaman Lamine Zeine, anachukua nafasi yake Mahamadou Ouhoumoudou, ambaye alikuwa barani Ulaya wakati wa mapinduzi hayo.

Zeine, alihudumu katika wizara ya fedha nchini Niger tangu mwaka wa 2001 hadi wakati serikali ya rais wa zamani Mamadou Tandja ilipoangushwa na jeshi mwaka wa 2010.

Uteuzi huo umetangazwa kupitia televisheni inayomilikiwa na serikali ya Télé Sahel na msemaji wa jeshi nchini Niger.

Zeine amewahi kufanya kazi katika benki ya maenedeleo ya Afrika nchini Chad, Ivory Coast na Gabon.

Jeshi pia limemteua Brig Jenerali Amadou Didilli kama mkuu wa mamlaka ya juu ya ujumuishaji wa amani nchini humo (HACP) na Brig Jenerali Abou Tague Mahamadou kama mkaguzi mkuu wa jeshi na jeshi la kitaifa.

Alimtaja Kanali Ibro Amadou Bachirou kuwa mkuu wa wafanyikazi wa kibinafsi wa kiongozi wa jeshi  na luteni Kanali Habibou Assoumane kama kamanda wa walinzi wa rais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.