Pata taarifa kuu

MONUSCO yalaani mauaji ya raia huko Murangara mashariki mwa DRC

NAIROBI – Mkuu wa Tume ya Umoja wa mataifa ya kulinda amani nchini DRC MONUSCO, Bintou Keita, amelaani vikali mashambulio dhidi ya raia huko Murangara katika Mkoa wa Kivu Kaskazini, ambapo watu 11 waliuawa na wengine wanne walijeruhiwa.

Mkuu wa Monusco nchini DRC, Bintou Keita akihutubia wanahabari kuhusu mchakato wa mpito wa pamoja wa Serikali-MONUSCO na changamoto za usalama mashariki mwa DRC, Agosti 3, 2023.
Mkuu wa Monusco nchini DRC, Bintou Keita akihutubia wanahabari kuhusu mchakato wa mpito wa pamoja wa Serikali-MONUSCO na changamoto za usalama mashariki mwa DRC, Agosti 3, 2023. Β© @UN_BintouKeita
Matangazo ya kibiashara

Bintou ameyataka makundi yote yenye silaha kukubali kusalimisha silaha zao na kujiunga na Mpango wa PDDRC-S.

Kwa mujibu wa mashirika ya kiraia pamoja na mashuhuda wengine, vifo hivyo viliripotiwa baada ya waasi wa kundi la M23 waliposhambulia ngome inayodhibitiwa na makundi ya wapiganaji wenye silaha, hususan Nyatura CMC katika eneo hilo la Murangara mwishoni mwa juma lililopita.

Ripoti zinasema mapigano hayo yalisababisha raia wachache kukimbia makazi yao, katika maeneo hayo ya Murangara na Runzenze huko Tongo, yakiwa chini ya udhibiti wa makundi yenye silaha ya Nyatura CMC na NDC\RΓ©novΓ© walikuwa na udhibiti wa Murangara.

Bintou Keita kupitia akaunti ya twitter ya MONUSCO, ambayo sasa inaitwa X ametoa wito kwa makundi yote yenye silaha kusitisha mara moja uhasama.

Kadhalika ameyataka makundi hayo kuweka silaha chini bila masharti na kuzingatia mpango wa kupokonywa silaha, kuhamishwa na kuingizwa katika Jamii maarufu kama (PDDRC-S).

Keita amesema kwamba wakiheshimu hatua hiyo, watakuwa wameokoa maisha ya raia wengi katika eneo hilo la mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC.

Wito huu unajiri wakati huu majeruhi wakiendelea kuhudumiwa katika hospitali ya Rutshuru na ile ya Bambo.

Ripoti imeandaliwa na Ruben Lukumbuka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.