Pata taarifa kuu

Raia wa Jamhuri ya Afrika ya kati wapitisha marekebisho ya katiba

Nairobi – Matokeo ya awali Iliyotolewa na kamati inayosimamia kura ya maoni nchini Jamhuri ya Afrika ya kati yameonyesha kuwa Idadi kubwa ya watu wameidhinisha mabadiliko ya katiba ya kwa zaidi ya asilimia 95 ya kura.

Asilimia 95 ya raia nchini humo waliunga mkono mchakato huo
Asilimia 95 ya raia nchini humo waliunga mkono mchakato huo AFP - BARBARA DEBOUT
Matangazo ya kibiashara

Baadhi ya vyama vya upinzani na wawakilishi wachache wa mashirika ya kiraia waliisusia kura hiyo, wengi wao wakisema kuwa mabadiliko hayo yanalenga kumpa muhula wa tatu Rais Faustin-Archange Touadéra na uwezekano wa kusalia madarakani zaidi maisha yake yote.

Wakosoaji wengine wanasema kura hiyo ya maoni iliyofanyika hivi karibuni nchini humo, imekosa uwazi na kwamba muda uliotolewa kujadili vifungu vya katiba hiyo ulikuwa ni mfupi.

Sheria inayopendekezwa inafuta ukomo wa mihula miwili ya urais ambapo rais atatakiwa kukaa madarakani kwa muda wa miaka saba badala ya miaka mitano kama ilivyokuwa awali, na pia inapiga marufuku wanasiasa wenye uraia wa nchi mbili kugombea urais.

Kutakuwa na ofisi ya makamu wa rais, ambayo itateuliwa rais mwenywe, huku Bunge la seneti litafutiliwa mbali, na kubadilisha bunge kuwa moja.

Idadi ya majaji wa mahakama kuu imeongezwa kutoka tisa hadi 11.

Takribani watu milioni mbili walijiandikisha kupiga kura, na waliojitokeza walikadiriwa kuwa wachache.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.