Pata taarifa kuu

Ethiopia: Mapigano jimboni Amhara yanaathiri utoaji wa misaada

Nairobi – Nchini Ethiopia, mapigano yanayoshuhudiwa katika jimbo la Amhara, kati ya waasi wenye silaha na jeshi la serikali yanaathiri pakubwa shughuli za utoaji misaada ya binadamu. 

WHO inasema kufungwa  kwa barabara kumeathiri utoaji wa misaada
WHO inasema kufungwa kwa barabara kumeathiri utoaji wa misaada © AFP
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa Shirika la afya duniani WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema, kufuatia kufungwa kwa barabara ni vigumu kwa misaada muhimu hasa ya afya, kuwafikia raia wa kawaida, lakini pia kuzimwa kwa mtandao wa Internet, unatatiza juhudi za mawasiliano. 

Mapigano katika jimbo la Amhara, yamekuja, miezi tisa baada ya kumalizika kwa vita vya miaka miwili kati ya waasi wa jimbo la Tigray na wanajeshi wa serikali. 

Kutokana na kuendelea kwa vita hivyo, waziri mkuu Abiy Ahmed ametanagza hali ya dharura katika jimbo hilo, huku serikali ikisema imewakamata watu wanaodaiwa kuchochea machafuko hayo. 

Tangu mwezi Aprili, hali ya wasiwasi ilianza kushuhudiwa baada ya serikali jijini Addis Ababa kuanza operesheni ya kuwapokonya silaha na kuyavunja makundi ya ulinzi katika majimbo ya nchi hiyo, hatua ambayo ilipinga na kundi linapokatikana kwenye jimbo la Amhara. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.