Pata taarifa kuu
TAARIFA

RFI na France 24 zakasirishwa na kusitishwa kwa matangazo yao nchini Niger

Wiki moja baada ya mapinduzi ya kijeshi nchini Niger, kulingana na vyanzo kadhaa nchini humo, matangazo ya vipindi vya RFI na France 24 yamesitishwa nchini humo.  Taasisi ya France Médias Monde, inayojumuisha vyombo vya habari vya kimataifa vya Ufaransa ikiwa ni pamoja na RFI, France 24 na Monte Carlo Doualiya inashutumu uamuzi huu uliochukuliwa nje ya mfumo wowote wa kawaida na wa kisheria, ambao unawanyima raia katika eneo hilo ufikiaji wao wa habari huru, iliyofanyiwa uchunguzi wa kina. 

RFI
RFI © RFI/Sébastien Bonijol
Matangazo ya kibiashara

Wakati RFI na France 24 tayari zimekabiliwa na udhibiti nchini Mali na Burkina Faso katika miezi ya hivi karibuni, kikundi hicho kinakumbusha kushikamana kwake na uhuru wa habari, wingi wa habari, pamoja na kazi ya kitaaluma na usalama wa waandishi wa habari.

Nchini Niger, RFI ina mitambo 7 ya masafa ya FM, pamoja na masafa mafupi ambayo yanatangaza programu zake kwa Kifaransa, Hausa na Fulfulde, pamoja na upatikanaji kwenye satelaiti kadhaa (hususan kwenye setilaiti ya SES 5, Eutelsat 16A na SES 4). Mtandao wa redio washirika pia hutangaza vipindi vyake kwa Kifaransa, Kihausa na Fulfulde. Mnamo 2022, wasikilizaji milioni 1.9 walisikiliza redio kila wiki nchini Niger (18% ya idadi ya watu) na ilikuwa redio ya kwanza ya kimataifa ikitoa nafasi kwa viongozi na raia mbalimbali. France 24 iliangaliwa na robo ya wakazi wa Niger kila wiki.

RFI na France 24 kwa sasa bado zinasikika na kuangaliwa nchini Niger kwenye mitambo ya mapokezi ya satelaiti ya moja kwa moja kwenye:

SES-5: RFI katika Kifaransa, Hausa, Fulfulde, Mandenkan na Kiswahili; France 24 kwa Kifaransa na Kiingereza

Eutelsat 16A: RFI na France 24 kwa Kifaransa

Arab-Sat/Badr: France 24 kwa Kifaransa, Kiingereza na Kiarabu; RFI kwa Kifaransa

Vipindi vya RFI katika Kifaransa, Kihausa na Fulfulde vinaendelea kutangazwa kwenye masafa mafupi.

RFI na France 24 pia zinapatikana kwenye YouTube, kwenye appli zao, tovuti zao na mitandao ya kijamii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.