Pata taarifa kuu

Niger: Emmanuel Macron azungumza na Bazoum, ambaye anasema 'yuko katika afya njema'

Siku mbili baada ya jeshi kuchukua mamlaka nchini Niger, Ufaransa, kupitia Catherine Colonna, Waziri wake wa Mashauri ya Kigeni, inafahamisha kwamba haizingatii mapinduzi ya "jaribio" kuwa yamefikia 'mwisho'.

Rais wa Niger Mohamed Bazoum, wakati wa mahojiano yake na RFI na France 24, Septemba 22, 2022.
Rais wa Niger Mohamed Bazoum, wakati wa mahojiano yake na RFI na France 24, Septemba 22, 2022. © RFI/France 24
Matangazo ya kibiashara

Rais Emmanuel Macron amezungumza mara kadhaa na mwenzake wa Niger  Mohamed Bazoum, anayezuiliwa mjini Niamey, ambaye amemwambia kuwa 'yuko katika afya njema', waziri wa mambo ya Nje wa Ufaransa, amefahamishwa kando ya ziara ya Rais Macron nchini Papua New Guinea.

Hayo yanajiri wakati operesheni za kibinadamu za Umoja wa Mataifa nchini Niger "zimesitishwa", kufuatia mapinduzi ya kijeshi kulingana na msemaji wa Umoja wa Mataifa Stéphane Dujarric.

Rais wa Niger Mohamed Bazoum alitoa ujumbe siku ya Alhamisi wa kuonesha ukaidi kwenye Twitter baada ya wanajeshi kutangaza mapinduzi katika taifa hilo la Afrika Magharibi.

Rais huyo mwenye umri wa miaka 64, ambaye alichaguliwa kuwa rais wa Niger miaka miwili iliyopita, aliandika kwenye mtandao wa Twitter siku ya Alhamisi asubuhi na kusema: "Mafanikio yaliyopatikana kwa bidii yatalindwa. Wananchi wote wa Niger wanaopenda demokrasia na uhuru watashuhudia hilo."

Waziri wake wa mambo ya nje alisema mapinduzi hayo hayaungwi mkono na jeshi zima, lakini mkuu wa jeshi sasa amesema anaunga mkono utawala wa kijeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.