Pata taarifa kuu

Tunisia: HRW imewatuhumu polisi kwa kukiuka haki za wahamiaji weusi

Nairobi – Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Human Rights Watch (HRW) limewatuhumu maofisa wa usalama nchini Tunisia kwa ukiukaji wa haki za  wahamiaji weusi  wanaojaribu kuvuka kuingia barani Ulaya.

HRW inawathumu polisi nchini Tunisia kwa kuwahangaisha wahamiaji weusi
HRW inawathumu polisi nchini Tunisia kwa kuwahangaisha wahamiaji weusi AP - Hassene Dridi
Matangazo ya kibiashara

HRW linasema limewahoji zaidi ya wahamiaji 20 na waomba hifadhi tangu mwezi Machi.

Saba kati yao walikuwa miongoni mwa zaidi ya  wahamiaji weusi waliofukuzwa au kusafirishwa kwa ulazima na mamlaka ya Tunisia hadi kaktika mpaka wa nchi hiyo na Libya au Algeria mwezi huu.

Rais Kais Saied amewatuhumu waandamanaji kuhusika na machafuko na ugaidi.

HRW inataka Umoja wa Ulaya kuzuia ufadhili ambao ungetumika kuwarejesha nyumbani wahamiaji hao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.