Pata taarifa kuu

Sudan: Watu 34 wameuawa katika shambulio mjini Omdurman

Nairobi – Nchini Sudan, maofisa katika idara ya afya wanaeleza kwamba watu 34 wakiwemo watoto wameuawa katika kile wamekitaja kuwa shambulio kwenye soko katika mji wa Omdurman.

Mojawapo ya mitaa katika mji wa Omdurman, Sudan ambapo mapigano yamekuwa yakiripotiwa
Mojawapo ya mitaa katika mji wa Omdurman, Sudan ambapo mapigano yamekuwa yakiripotiwa AFP
Matangazo ya kibiashara

Licha ya taarifa hiyo, haijabainika ni nani aliyetekeleza shambulio hilo la Jumanne.

Watu wengine 45 waliuawa katika shambulio la anga siku ya Jumamosi kwenye mji huo unaopakana na mto Nile kutoka jiji kuu, Khartoum.

Mapigano kati ya jeshi la Sudan na wapiganaji wa RSF yamekuwa yakiendelea kwa miezi mitatu sasa.

Makabiliano kati ya pande hizo mbili yameripotiwa kusababisha vifo vya watu elfu tatu wakati maelfu ya wengine wakiwa wametoroka makazi yao.

Mataifa jirani na Sudan kama vile Chad na Sudan Kusini yameendelea kupokea idadi kubwa ya wakimbizi wanaotoroka vita nchini mwao.

Pande hasimu nchini Sudan zimeendelea kupigana licha ya wito kutolewa kutoka kwa jamii ya kimataifa wa kutaka vita hivyo kusitishwa.

Miundo mbinu kama vile barabara, hosipitali imeripotiwa kuharibiwa katika makabiliano hayo, wanajeshi wa serikali wakiwatuhumu wapiganaji wa RSF kwa kutekeleza uharibifu huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.