Pata taarifa kuu

Rais wa Iran, Ebrahim Raisi anazuru Kenya

Nairobi – Rais wa Iran, Ebrahim Raisi, ameanza ziara yake barani Afrika kwa kutembelea nchi ya Kenya kicha Uganda na baadae Zimbabwe, ziara ambayo wadadisi wa mambo wanasema Tehran inajaribu kutafuta ushawishi wake na mataifa ya Afrika.

Kiongozi huyo alitarajiwa kuwasili Kenya Jumanne lakini ziara yake iliarishwa hadi leo Jumatano
Kiongozi huyo alitarajiwa kuwasili Kenya Jumanne lakini ziara yake iliarishwa hadi leo Jumatano © Alfred Mutua
Matangazo ya kibiashara

Hii itakuwa ni ziara ya kwanza kufanywa na kiongozi wa taifa hilo katika kipindi cha miaka karibu 11, ambapo anatarajiwa kutia saini makubaliano kadhaa ya ushirikiano wa kiuchumi na kisiasa na mataifa hayo.

Ziara hiyo ilikuwa imepangwa kufanyika siku ya Jumanne lakini ilicheleweshwa hadi leo Jumatano nchi za Kenya na Iran zikitoa maelezo yasiyo wazi kuhusu mabadiliko hayo.

Wizara ya mambo ya nje ya Kenya baadae ikatoa tarifa fupi ikisema safari hiyo ilichelewesha hadi jumatano asubuhi,kutoa nafasi zaidi kukamimishwa kwa mikataba ambayo nchi ya Kenya na Iran ilitakiwa kusaini.

Ebrahim Raisi ni kiongozi wa pili, kufika Kenya baada ya Rais wa zamani, Mahmoud Ahmadinejad kutembelea Kenya mwaka 2009 akiwa rais wa Kwanza wa Iran kuzuru Kenya.

Haji Kaburu ni mchambuzi wa siasa za kimataifa akiwa Tanzania hapa anatoa tathmini yake kuhusu ziara hii.

‘‘Nadhani China, Urusi, Iran zote zinatafuta nafasi ya kuingia barani Afrika na fursa ambayo wengi walikuwa wameiona haitapatikana kutokana na suala kwamba zile nchi za magharibi zilikuwa zimetawala Afrika.’’ amesema Haji Kaburu ni mchambuzi wa siasa za kimataifa.

00:36

Haji Kaburu ni mchambuzi wa siasa za kimataifa akiwa Tanzania

Hivi karibuni Iran imeanza kuimarisha diplomasia yake na mataifa kadhaa hasa baada ya vikwazo vya Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.