Pata taarifa kuu

Vita nchini Sudan vinatishia kugeuka kuwa vya wenyewe kwa wenyewe: UN

Umoja wa Mataifa, unaonya kuwa vita vinavyoendelea nchini Sudan kati ya wanajeshi na wanamgambo wa RSF vinatishia kugeuka kuwa vya wenyewe kwa wenyewe, vinavyoweza kutikisa nchi za ukanda.

Mapigano yameendelea kuripotiwa nchini Sudan licha ya wito wa kusitishwa kuendelea kutolewa
Mapigano yameendelea kuripotiwa nchini Sudan licha ya wito wa kusitishwa kuendelea kutolewa © AFP
Matangazo ya kibiashara

Onyo hili limetolewa baada ya ndege za kijeshi, kushambulia makaazi ya watu na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 20.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, amelaani shambulio hilo lilitokea kwenye mji wa Omdurman, ambaye ameongeza kuwa iwapo vita vinavyoendelea havitakoma, ukanda  mzima upo kwenye hatari ya kuathiriwa.

Imepita sasa miezi tatu tangu kuanza kwa mapigano hayo na juhudi za Kimataifa kujaribu kuzileta pamoja, pande mbili zinazopigana, zimeambulia patupu.

Mpaka sasa watu zaidi ya Elfu tatu wameuawa kwenye mzozo huu, huku kukiwa na ripoti za wanawake na wasichana kubakwa. Umoja wa Mataifa unaonya kuwa visa vya uhalifu wa kivita, vinaendelea katika jimbo la Darfur.

Wanamgambo wa RSF wamejenga kambi zao katika makaazi ya watu na kusababisha raia wa kawaida kuyakimbia makaazi yao, wakati huu takwimu za Umoja wa Mataifa zikieleza kuwa watu Milioni Tatu wameyakimbia makwao, wakiwemo Laki Saba waliokimbilia kwenye nchi jirani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.