Pata taarifa kuu

Watu karibia milioni tatu wametoroka mapigano nchini Sudan: IOM

Nairobi – Karibu watu milioni 3 wamekimbia makazi yao na wengine kuvuka mpaka kutokana na mzozo unaoendelea nchini Sudan katika kipindi cha chini ya miezi mitatu, limesema shirika linalohusika na wahamiaji, IOM.

Mapigano nchini Sudan yamewalazimu raia kutorokea katika baadhi ya mataifa jirani wakihofia kushambuliwa
Mapigano nchini Sudan yamewalazimu raia kutorokea katika baadhi ya mataifa jirani wakihofia kushambuliwa AP
Matangazo ya kibiashara

Takwimu zinaonyesha asilimia 67 ya raia wamekimbia kutoka mji wa Khartoum, asilimia 33 kutoka Darfur na asilimia nyingine kutoka majimbo ya Mto Nile, White Nile miongoni mwa sehemu zingine.

Uchunguzi umeonyesha kuwa, wengi wa raia hao wamevuka na kuingia nchi jirani ya Misri kwa asilimia 40, wengine Chad, Sudan Kusini, Ethiopia na Jamhuri ya Afrika ya Kati na asilimia kubwa ya waliovuka ni raia wa Sudan.

Kuendelea kwa vurugu nchini humo kumesababisha hali mbaya ya kibinadamu haswa chakula na huduma za afya, wakati huu mkurugenzi wa ukanda wa IOM MENA, Othman Belbeisi, akisisitiza wito wa kusitishwa mapigano.

Nchini Sudan, shehena ya misaada imewasili katika bandari ya Sudan ili kusambazwa kupitia washirika, IOM ikihitaji ufadhili zaidi wa haraka ili kuendeleza shughuli hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.