Pata taarifa kuu

DR Congo na Afrika kusini zimetia saini ujenzi wa bwawa la umeme

Wakuu wa nchi za Afrika Kusini na Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, wametia saini karibia makubaliano 40 kuhusu biashara yakiwemo yale yanayohusu mpango wa kufufua mradi wa kujenga mabwawa mengi kwenye mto Congo

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa na mwenzake wa DRC  Félix Tshisekedi
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa na mwenzake wa DRC Félix Tshisekedi REUTERS - JUSTIN MAKANGARA
Matangazo ya kibiashara

Mradi wa bwawa kubwa la  Inga ni miongoni mwa  wa vituo saba vya kuzalisha umeme vinavyopendekezwa kujengwa katika mto Kongo.

Iwapo mradi huo utafanikishwa kama ilivyopangwa, utakuwa ni mojawapo ya miradi mikubwa zaidi duniani.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alitia saini makubaliano hayo na mwenzake Felix Tshisekedi jijini Kinshasa nchini DR Congo,.

Afrika Kusini inakabiliwa na tatizo kubwa la umeme kutokana na kukatika kwa umeme mara kwa mara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.