Pata taarifa kuu

Afrika Kusini: Uvujaji wa gesi katika makazi duni waua watu 16

Watu kumi 17, wakiwemo watoto, walifariki Jumatano jioni baada ya gesi kuvuja katika kitongoji duni cha Boksburg, kilomita zaidi ya 40 mashariki mwa Johannesburg, kulingana na idara ya huduma za dharura nchini Afrika Kusini.

Uvujaji wa gesi ulitokana na mtungi wa oksidi ya nitrate, ambayo ingetumika "katika mazingira ya shughuli haramu za uchimbaji madini", kulingana na wachunguzi.
Uvujaji wa gesi ulitokana na mtungi wa oksidi ya nitrate, ambayo ingetumika "katika mazingira ya shughuli haramu za uchimbaji madini", kulingana na wachunguzi. © WIKUS DE WET / AFP
Matangazo ya kibiashara

Uvujaji wa gesi unatokana na mtungi wa oksidi ya nitrate, ambayo ingetumika "katika mazingira ya shughuli haramu za uchimbaji madini", kulingana na wachunguzi.

"Tumethibitisha vifo vya watu 16 katika eneo la tukio", watu wanane, wanawake watano na watoto watatu, msemaji wa idara ya huduma za dharura William Ntladi ameliambia shirika la habari la AFP, na kuongeza kuwa wengine 16 wamejeruhiwa.

Awali idara ya huduma za dharura ilitangaza kuwa watu 24 walifariki katika mkasa huo, saa chache kabla ya kurekebisha idadi hiyo na kusema kuwa watu 16 ndio waliofariki.

Miongoni mwa waliojeruhiwa, "wanne wamelazwa hospitalini wakiwa katika hali mbaya, kumi na moja wanaendelea vizuri" na wa mwisho, mtoto mdogo, "sasa yuko sawa", idara ya huduma za dharura imebaini katika taarifa yake.

Baada ya kupigiwa simu karibu saa mbili usiku, kwa kile kilichoonekana kuwa mlipuko, idara ya huduma za dharura ziligundua kuwa ni uvujaji wa gesi. Mtungi wa oksidi ya nitrate ulipatikana katika eneo la tukio.

"Tulipofika, tuliona makumi ya watu wamelala katika eneo la tukio kutokana na kuvuta gesi hii yenye sumu," amesema msemaji wa idara ya huduma za dharura.

“Taarifa za awali zinaonyesha kuwa watu hawa walikuwa wakitumia gesi hii katika mazingira ya shughuli haramu za uchimbaji madini,” William Ntladi ameliambia shirka la habari la AFP. "Inavyoonekana wachimbaji walikuwa wakitumia gesi kuchimba dhahabu kutoka ardhini."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.