Pata taarifa kuu

Uamuzi wa rais wa Senegal ni 'mfano kwa kanda nzima', kulingana na Marekani

Marekani 'imekaribisha' tangazo la rais wa Senegal Macky Sall kutowania muhula wa tatu mwezi Februari 2024, uamuzi ambao wanasema unaonyesha "mfano kwa kanda nzima".

Rais aw Senegal Macky Sall wakati wa mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika mnamo Februari 18, 2022.
Rais aw Senegal Macky Sall wakati wa mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika mnamo Februari 18, 2022. AP - John Thys
Matangazo ya kibiashara

"Tangazo la wazi la rais Sall linatoa mfano kwa kanda hiyo, tofauti na wale wanaotaka kuharibu kanuni za kidemokrasia, ikiwa ni pamoja na ukomo wa muhula," Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani amesema Anthony Blinken katika taarifa.

"Tunaamini kuwa uchaguzi huru na wa haki na mpito wa mamlaka hufanya taasisi kuwa imara na nchi zenye utulivu na ustawi," ameongeza.

Amesema Marekani "inajivunia kuunga mkono taasisi za uchaguzi za Senegal," na ameahidi "kuendelea kufanya kazi na Senegal kuunga mkono dhamira thabiti ya raia wa Senegal katika demokrasia."

Senegal inachukuliwa kuwa mshirika mkuu wa Marekani, Marekani hivi karibuni ilionyesha nia yake ya kuimarisha uhusiano wake na nchi za Afrika.

Joe Biden aliandaa mkutano wa kilele huko Washington mnamo Desemba 2022 ukiwaleta pamoja baadhi ya viongozi hamsini kutoka bara hilo, akiwemo Rais Macky Sall.

Wakati huo huo Ufaransa pia imekaribisha uamuzi wa rais Macky Sall wa kutogombea tena kiti cha urais katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2024.

"Senegal kwa mara nyingine tena inadhihirisha uimara wa utamaduni wake wa muda mrefu wa kidemokrasia," amesema François Delmas, naibu msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa katika taarifa kwa vyombo vya habari, iliyochapishwa Jumanne Julai 4.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.