Pata taarifa kuu

Afrika Kusini: Mfalme wa Kizulu afanyiwa vipimo baada ya kifo cha cha mshauri wake

Mfalme wa Wazulu, mtawala wa kitamaduni mwenye nguvu zaidi nchini Afrika Kusini, alifanyiwa vipimo "vyaa kina" baada ya kifo cha ghafla cha mmoja wa washauri wake wa karibu, na yuko "katika afya njema", msemaji wake alisema Jumapili, wakati sauti zingine kutoka kasri la mfalme zikibaini kwamba kuna uwezekano kuwa viongozi hao walipewa sumu.

Mfalme wa Taifa la Amazulu, Misuzulu kaZwelithini (katikati) akiwa ameshika mkuki anapoimba pamoja na Amabutho (watawala wa Kizulu) wakati wa kutawazwa kwake katika Kasri la Kifalme la KwaKhangelamankengane huko Kwa-Nongoma kilomita 300 kaskazini mwa Durban mnamo Agosti 20, 2022.
Mfalme wa Taifa la Amazulu, Misuzulu kaZwelithini (katikati) akiwa ameshika mkuki anapoimba pamoja na Amabutho (watawala wa Kizulu) wakati wa kutawazwa kwake katika Kasri la Kifalme la KwaKhangelamankengane huko Kwa-Nongoma kilomita 300 kaskazini mwa Durban mnamo Agosti 20, 2022. AFP - PHILL MAGAKOE
Matangazo ya kibiashara

"Mfalme, alipokuwa ziarani nchini Eswatini, alifanyiwa uchunguzi wa kina wa kimatibabu kama tahadhari katika muktadha wa Uviko na baada ya kifo cha ghafla cha mshauri wake wa karibu," amesema Mwanamfalme Africa Zulu, aliyehojiwa kwa simu na shirika la habari la AFP.

Amehakikisha kwamba Misuzulu Zulu, 48, ambaye pia anaitwa Misuzulu kaZwelithini, "yu mzima wa afya njema na kwamba kwa sasa hajalazwa katika hospitali yoyote", msemaji wa mfalme alikashifu katika taarifa kwa vyombo vya habari "jaribio lililopangwa" la kusambaza habari "isiyo na msingi" kuhusu afya ya mfalme".

Katika taarifa iliyotolewa usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili, Waziri Mkuu mwenye ushawishi wa kimila wa Kizulu, Mangosuthu Buthelezi, alisema aliarifiwa kwamba Misuzulu Zulu amelazwa hospitalini "baada ya kuugua mapema asubuhi" siku ya Jumamosi.

Kulingana na mwakilishi huyu anayeheshimika wa familia ya kifalme ya Wazulu, mfalme aliamini kuwa kuna uwezekano wa kuwekewa sumu baada ya kifo cha ghafla na cha ajabu cha mshauri wake siku ya Jumamosi.

Douglas Xaba "alifariki ghafla na inashukiwa kuwa alilishwa sumu", alieleza Bw Buthelezi. "Wakati mfalme wake alipoanza kujisikia vibaya, alishuku kuwa yeye pia alikuwa amepewa sumu."

Mfalme alipendelea kwenda kuhudumiwa kimatibabu nchini Eswatini badala ya Afrika Kusini ambako wazazi wake wote "walitibiwa na kufariki", aliongeza, akielezea "wasiwasi wake mkubwa".

Vyanzo kadhaa vya polisi huko Eswatini vimelithibitishia shirika la habari la AFP kupelekwa kwa idadi kubwa ya vikosi vya usalama katika hospitali ya kibinafsi ya Ezulwini, kilomita chache kutoka kwa makazi ya mfalme wa Eswatini, mfalme wa mwisho kabisa barani Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.