Pata taarifa kuu

Ethiopia yaomba kujiunga na muungano wa BRICS

Nairobi – Nchi ya Ethiopia, ambayo ni miongoni mwa nchi zinazokuwa kwa kasi zaidi kiuchumi barani Afrika, imeomba kujiunga jumuiya ya masoko yanayoibuka, BRICS, inayojumuisha nchi za Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed. AP - Mulugeta Ayene
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo ya nje nchini Ethiopia Meles Alem amesema wanatarajia kupata majibu chanya kwa ombi lao, na kwamba Ethiopia itaendelea kufanya kazi na taasisi za kimataifa zinazoweza kulinda maslahi yake.

Taifa hilo la pembe ya Afrika kwa sasa ni  la pili kwa idadi kubwa ya watu barani Afrika, lakini kwa mujibu wa shirika la fedha duniani IMF, uchumi wake uko katika nafasi ya 59 duniani, ukiwa chini ya nusu ya ule wa nchi ya Afrika Kusini ambayo ni  mwanachama wa BRICS.

Alhamis ya wiki hii, Afrika Kusini ilitangaza kuwa mwenyeji wa mkutano ujao wa jumuiya hiyo mwezi Agosti, wakati huu kukiwa na uvumi kuwa huenda mkutano ukahamishwa katika eneo ambapo rais wa urusi Vladimir Putin hawezi kukamatwa kwa tuhuma za uhalifu wa kivita.

Nchi za BRICS zinachangia jumla ya zaidi ya asilimia 40 ya watu duniani na karibu asilimia 26 ya uchumi wa dunia.

Neno BRIC lilibuniwa na mwanauchumi wa kampuni ya Goldman Sachs Jim O'Neill mwaka wa 2001 kuelezea kukua kiuchumi kwa nchi za Brazil, Russia, India na China.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.