Pata taarifa kuu

Sudan: Zaidi ya wafungwa 100 wa kivita wameachiwa huru: ICRC

Nairobi – Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu (ICRC) inasema ilifanya upatanishi kati ya pande zinazozozana nchini Sudan ili kuwezesha kuachiliwa kwa zaidi ya wafungwa 100 wa kivita.

Mapigano yamekuwa yakiendelea nchini Sudan licha ya wito wa kusitishwa
Mapigano yamekuwa yakiendelea nchini Sudan licha ya wito wa kusitishwa REUTERS - MOHAMED NURELDIN ABDALLAH
Matangazo ya kibiashara

Sudan imekumbwa na ghasia tangu Aprili 15 wakati mzozo wa kuwania madaraka kati ya wakuu wa jeshi la Sudan na wapiganaji wa  RSF ulipoaanza na kusababisha vita vikali vilivyosababisha vifo vya maelfu ya watu na kuwalazimisha mamilioni ya watu kuyahama makazi yao.

Katika ripoti yake ICRC,  jumla ya wanajeshi 125 wanaoshikiliwa na RSF waliwezeshwa kurejea kwa familia zao kabla ya Eid al-Adha. Miongoni mwa walioachiwa huru, 44 walikuwa wamejeruhiwa. Kundi hilo lilichukuliwa kutoka Khartoum hadi Wad Madani, kusini mwa mji mkuu.

Majeruhi wengine 14 waliachiliwa siku ya Jumatatu kwa usaidizi wa ICRC katika eneo la Darfur, magharibi mwa nchi hiyo.

Wiki hii, jeshi la Sudan na RSF walitangaza kusitisha mapigano kwa ajili ya Eid al-Adha, lakini wakaazi wa Khartoum, hatua ambayo wakaazi wa jiji hilo walisema hayana maana huku kukiwa na ripoti za mashambulio ya makombora.

Mikataba mingi ya kusitisha mapigano imeshindwa kudumu, ikiwa ni pamoja na kadhaa iliyosimamiwa na Saudi Arabia na Marekani katika mazungumzo yaliyositishwa katika mji wa bandari wa Saudi wa Jeddah.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.