Pata taarifa kuu

Sudan : Pande hasimu zatuhumiana kwa kushambulia raia

Nairobi – Pande zinazohasimiana nchini Sudan, zimeendelea kutupiana lawama kila mmoja akidai mwenzake ndiye anashambulioa raia, wakati huu milipuko na milio ya risasi ikishuhudiwa kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Khartoum.

Generali Fattah al-Burhan, Mkuu wa jeshi la Sudan
Generali Fattah al-Burhan, Mkuu wa jeshi la Sudan via REUTERS - SUDANESE ARMED FORCES
Matangazo ya kibiashara

Wakaazi wa Khartoum wamesema, wameshuhudia magari ya kijeshi yakirusha risasi na makombora katika mitaa wanakoishi watu, Kaskazini mwa mji huo.

Tangu kuanza kwa vita hivyo miezi miwili iliyopita, pande hizo mbili zimeendelea kulaumiana kwa kusababisha vifo vya raia wa kawaida. Tume ya Umoja wa Mataifa, inasema watu zaidi ya Elfu Mbili wameuawa mpaka sasa.

Maelfu ya watu wameendelea kuteseka, kwa kukosa mahitaji muhimu ya kibinadamu kama dawa na chakula, huku huduma muhimu kama maji na umeme zikikatwa.

Siku ya Jumatatu, katika kongamano la wahisani jijini Geneva, ahadi ya kukusanya Dola Bilioni 1.5 ilitolewa kuwaisaidia raia wa Sudan ambao wanahitaji misaada ya kibinadamu kwa haraka.

Tume ya Umoja wa Mataifa kuhusu wakimbizi inasema vita nchini Sudan vimewaathiri watu Milioni 25 huku wengine 600,000 wakikimbilia katika mataifa jirani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.