Pata taarifa kuu

Ujumbe wa wapatanishi kutoka Afrika umewasili Ukraine kabla ya kuelekea Urusi

NAIROBI – Viongozi wa Afrika hivi leo wamewasili nchini Ukraine kabla ya hapo kesho kuelekea Urusi, katika ziara inayolenga kujaribu kuwashawishi viongozi wa nchi hizo mbili kukubaliana kumaliza vita inayoendelea.

Viongozi hao wanajaribu kutafuta muafaka kati ya Ukraine na Urusi
Viongozi hao wanajaribu kutafuta muafaka kati ya Ukraine na Urusi © Presidency | South Africa
Matangazo ya kibiashara

Ujumbe huo wa viongozi wa Afrika, unaongozwa na rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, utakuwa na mazungumzo na rais Volodymry Zelenky na Vladimir Putin kwa nyakati tofauti.

Hata hivyo ni ziara iliyoibua hisia mseto ikiwa itafanikiwa. Liesl Louw Vaudran, ni mratibu wa shirika la kimataifa la utatuzi wa mizozo, ICG.

“Huu ni mpango muhimu unaovutia sana ambao ungeweza kuweka wazi msimamo wa Afrika kuhusu kinachoendelea licha ya kuwa ni baadhi ya viongozi wa nchi za Afrika ndio wanaoenda huko na huu sio mpango wa Afrika na pia naadhi ya nchi zilionesha kupinga uvamizi wa Urusi.’’ alisema Liesl Louw Vaudran, ni mratibu wa shirika la kimataifa la utatuzi wa mizozo, ICG.

00:37

Liesl Louw Vaudran, mratibu wa shirika la kimataifa la utatuzi wa mizozo, ICG

Ziara ya viongozi wa Afrika inakuja wakati huu nchi ya Marekani ikianusha madai ya Urusi kuwa Ukraine haijafanikiwa chochote katika operesheni za kijeshi ilizoanzisha juma hili, Washington ikisisitiza kuwa wanajeshi wa Kiev bado wanazana zakutosha kuvikabili vikosi vya Moscow na washirika wake.

Waziri wa ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin, amesema kinachofanya na Urusi ni propaganda kujaribu kuaminisha dunia kuwa bado inaudhibiti wa miji ambayo Ukraine imethibitisha kuichukua.

“Hivi ni vita na tunafahamu kwamba patakuwa na athari mbaya kwa pande zote, cha msingi, ni Ukraine iwe na uwezo wa kukarabati vifaa vinavyoharibiwa pale panapowezekana.’’alisema Lloyd Austin Waziri wa ulinzi wa Marekani.

00:27

Lloyd Austin Waziri wa ulinzi wa Marekani

Haya yanajiri baada ya Moswo kusambaza picha za video kuonesha imekamata vifaru vyakijrumani kutoka kwa wanajeshi wa Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.