Pata taarifa kuu

EU kuisaidia Tunisia kukabiliana na changamoto ya uhamiaji

NAIROBI – Ujumbe wa viongozi wa Ulaya umeahidi zaidi ya $1bn (£800m) kama msaada wa  kifedha kwa nchi ya Tunisia, kama sehemu ya mapendekezo mapana ya makubaliano yanayojumuisha hatua za kukabiliana na uhamiaji.

Tume ya umoja wa ulaya imeahidi kuisaidia nchi ya Tunisia kukabiliana na suala la uhamiaji
Tume ya umoja wa ulaya imeahidi kuisaidia nchi ya Tunisia kukabiliana na suala la uhamiaji AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa Tume ya Ulaya, Ursula von der Leyen, na mawaziri wakuu wa Italia na Uholanzi - Giorgia Meloni na Mark Rutte - wamekuwa wakifanya mazungumzo na Rais Kais Saied.

Von der Leyen alisema EU itaipatia Tunisia zaidi ya $100m mwaka huu kwa ajili ya usimamizi wa mipaka, utafutaji na uokoaji pamoja na kuwarejesha wahamiaji.

Alisisitiza pande zote mbili zilitaka kuvunja kile alichokiita mtindo wa biashara wa kijinga kuhusu usafirishaji wa watu.

Hata hivyo pendekezo kuhusu wahamiaji huenda lisikubaliwe na utawala wa Tunis, baada ya kauli ya rais Kais Saied aliyoitoa siku ya Jumamosi, ambapo alikataa nchi yake kuwa kituo cha kuzuia wakimbizi kwa nchi nyingine.

Msaada wa umoja wa Ulaya, umetangazwa licha ya ukanda huo kuukosoa utawala wa rais Kasi kwa kujaribu kuminya demokrasia kwa kuwakamata wakosoaji wake na kutawala kimabavu.

Haya yanajiri wakati huu, Tunisia ikiwa katika majadiliano na shirika la fedha duniani, IMF, kuhusu kupatiwa mkopo utakaosaidia kufufua uchumi wa taifa hilo

Rais Said ameshutumiwa na wakosoaji wa nyumbani na nje ya nchi kwa kurejesha taifa lake nyuma  kidemokrasia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.