Pata taarifa kuu

Ethiopia: Viongozi wa Amhara na Tigray kutatua changamoto zao kupitia mazungumzo

NAIROBI – Viongozi wa mikoa ya Amhara na Tigray nchini Ethiopia wameelezea kujitolea kwao kwa pamoja kutatua tofauti zao kupitia mazungumzo.

kiongozi wa muda wa Tigray, Getachew Reda
kiongozi wa muda wa Tigray, Getachew Reda AP
Matangazo ya kibiashara

Gavana wa eneo la Amhara Yilkal Kefale na kiongozi wa muda wa Tigray, Getachew Reda, walitoa ahadi hiyo wakati wa mazungumzo katika mji mkuu wa Amhara, Bahir Dar.

Getachew aliongoza ujumbe wa Tigray katika eneo la Amhara kwa mara ya kwanza tangu vita vikali vya wenyewe kwa wenyewe vilipozuka kaskazini mwa Ethiopia Novemba mwaka wa 2020.

Mapigano hayo yalimalizika baada ya kuafikiwa kwa makubaliano ya amani mwezi  Novemba mwaka jana.

Viongozi hao wawili walisema watafanya kazi ya kufungua tena usafiri wa barabara kati ya Tigray na Amhara, ambayo inarahisisha usafiri kati ya Tigray na Addis Ababa.

Kwa sasa, usafiri wa barabara kati ya Addis Ababa na Tigray kimsingi unapitia eneo la kaskazini-mashariki la Afar, ambalo ni refu na la gharama zaidi.

Hata hivyo, viongozi hao wawili hawakuzungumzia suala hilo la migogoro ya ardhi kati ya mikoa yao miwili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.